title : KAMPUNI YA JUMIA TZ YAZINDUA KAMPENI YA MAUZO YA BLACK FRIDAY
kiungo : KAMPUNI YA JUMIA TZ YAZINDUA KAMPENI YA MAUZO YA BLACK FRIDAY
KAMPUNI YA JUMIA TZ YAZINDUA KAMPENI YA MAUZO YA BLACK FRIDAY
Meneja wa Kampuni ya Skymark Nishit Modessa Akizungumzia ushiriki wao katika kampeni hiyo Kushoto ni Meneja Masoko wa Jumia Tanzania Albany James.
Afisa Masoko wa Jumia Tanzania Albany James akizungumzia uzinduzi rasmi wa kampeni kubwa ya mauzo ya mwaka inayojulikana kama BLACK FRIDAY inayolenga kuwawezesha watanzania kufanya manunuzi kwa ajili nya msimu wa sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya kupitia mtandao wa Jumia Tanzania, kulia ni Meneja Uhusiano wa Umma Jumia Tanzania Kijanga Geofrey.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam.
kampuni inayojihusisha na ununuzi wa bidhaa mtandaoni barani afrika ya wa Jumia Tanzania imezindua rasmi kampeni kubwa ya mauzo ya mwaka inayojulikana kama BLACK FRIDAY inayolenga kuwawezesha watanzania kufanya manunuzi kwa ajili nya msimu wa sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya kiurahisi zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam juu ya kampeni hiyo Meneja Masoko wa Jumia Tanzania Albany James amesema kuwa, kwa kawaida Black Friday imekuwa inafanyika kila mwaka ifikapo Novemba 23, lakini kwa mwaka huu itakuwa kila Ijumaa na itaanzia Novemba 23 mpaka Desemba 07 mwaka huu ambapo itawawezesha wateja kununua bidhaa mbali mbali kwa punguzo la bei hadi asilimia 70.
Aidha ameongeza kuwa tofauti na siku za kawaida za Black Friday kutakuwa na ofa nyingi zaidi na mapunguzo makubwa ya bei kwa bidhaa zote mpaka kufikia asilimia 70 na hii katika kuhakikisha wateja hawapitwi kunufaika na maununuzi ya bidhaa kutoka kwa wafanyabiashara tofauti wanaoaminika kwenye mtandao wa Jumia
."Ukiachana na ofa na mapunguzo ya bei, kutwakuwa na vocha za bure za manunuzi kuanzia shilingi 5,000 mpaka 80,000, mauzo ya bidhaa ya muda mfupi katika siku (flash sales) na kuogesha zaidi Black Friday kutakuwa na 'Treasure Hunt' kila Ijumaa ambapo bidhaa itafichwa kwenye mtandao wa Jumia,
"napenda kutoa wito kwa watanzania kuwa werevu kuwa werevu na kuitumia kampeni hii ya black friday ipasavyo kwa sababu bidhaa zote walizowahi kuzifikiria zitakuwa mbele ya macho yao kwa bei nafuu na wateja watakaofanya manunuzi ya zaidi ya 20,0000 watapelekewa bidhaa zao hadi sehemu walipo bila malipo''alisema James
Kwa upande wa washiriki wa Black Friday ambao wameingiza bidhaa zao za pikipiki na bajaji kuuzwa katika Jumia , Kutoka kampuni ya Skymark Meneja wa Kampuni hiyo, Nishit Modessa amesema kuwa wameamua kushirikiana na Jumia Tanzania baada ya kuona ni wazo zuri sana baada ya kuletewa na wakaamua kutoa pikipiki ili wateja wa Jumia washindanie.
Awali akizungumzia kuhusu kampeni hiyo meneja mahusiano wa Jumia Kijanga Geofrey amewataka watanzania kuionndoa hofu zao juu ya biashara kupitia mtandao kwa kusema kuwa mtandao wa Jumia umejizatiti katika kulinda wateja wake wanaonunua bidhaa kupitia mtandao sambamba na kuongeza kuwa wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kuyatafutia makampuni yanayouza bidhaa mbali mbali masoko ili kuwafikia wateja wake kiurahisi zaidi.
Hivyo makala KAMPUNI YA JUMIA TZ YAZINDUA KAMPENI YA MAUZO YA BLACK FRIDAY
yaani makala yote KAMPUNI YA JUMIA TZ YAZINDUA KAMPENI YA MAUZO YA BLACK FRIDAY Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMPUNI YA JUMIA TZ YAZINDUA KAMPENI YA MAUZO YA BLACK FRIDAY mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/kampuni-ya-jumia-tz-yazindua-kampeni-ya.html
0 Response to "KAMPUNI YA JUMIA TZ YAZINDUA KAMPENI YA MAUZO YA BLACK FRIDAY"
Post a Comment