title : HUKUMU KESI YA MATUMIZI MABAYA INAYOMKABILI TIDO MHANDO KUTOLEWA DESEMBA 18 ,2018
kiungo : HUKUMU KESI YA MATUMIZI MABAYA INAYOMKABILI TIDO MHANDO KUTOLEWA DESEMBA 18 ,2018
HUKUMU KESI YA MATUMIZI MABAYA INAYOMKABILI TIDO MHANDO KUTOLEWA DESEMBA 18 ,2018
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Desemba 18 mwaka huu inatarajia kutoa hukumu dhidi ya kesi ya matumizi mabaya ya madaraka inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando.
Katika kesi hiyo, Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh.milioni 887.1.
Hakimu Mkazi Mkuu,Huruma Shaidi anayesikiliza kesi hiyo, amefikia hatua hiyo baada ya Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa( Takukuru), Leonard Swai kuieleza Mahakama kuwa wamekwisha wasilisha majumuisho yao ya mwisho mahakamani hapo.
Naye Wakili wa utetezi wa Tido, Dk. Ramadhani Maleta ameiarifu Mahakama kuwa wakili mwenzake Martin Matunda ambaye walikuwa na wakimtetea Tido, amefariki dunia na lakini nao pia wamekwisha wasilisha hoja zao za mwisho.
Kutokana na taarifa hiyo Swai ameiomba Mahakama kuipangia Kesi hiyo tarehe ya hukumu ambapo Hakimu Shaidi amepanga kusoma hukumu hiyo Desemba 18, mwaka huu.Mwishoni mwa mwezi uliopita, Tido kupitia mawakili wake Martin Matunda na Dk Ramadhani Maleta walifunga ushahidi wa upande wa utetezi.
Katika kesi hiyo jumla ya mashahidi watatu wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo walitoa ushahidi na kufunga ushahidi wa upande wa mashtaka.Miongoni mwa mashahidi hao ni Afisa uchunguzi wa Takukuru, Victor Lesuya, Mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TBC, Clement Mshana.
Hivyo makala HUKUMU KESI YA MATUMIZI MABAYA INAYOMKABILI TIDO MHANDO KUTOLEWA DESEMBA 18 ,2018
yaani makala yote HUKUMU KESI YA MATUMIZI MABAYA INAYOMKABILI TIDO MHANDO KUTOLEWA DESEMBA 18 ,2018 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HUKUMU KESI YA MATUMIZI MABAYA INAYOMKABILI TIDO MHANDO KUTOLEWA DESEMBA 18 ,2018 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/hukumu-kesi-ya-matumizi-mabaya.html
0 Response to "HUKUMU KESI YA MATUMIZI MABAYA INAYOMKABILI TIDO MHANDO KUTOLEWA DESEMBA 18 ,2018"
Post a Comment