CUF YAMJIA JUU ALIEKUWA MBUNGE WA TEMEKE MTOLEA.

CUF YAMJIA JUU ALIEKUWA MBUNGE WA TEMEKE MTOLEA. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa CUF YAMJIA JUU ALIEKUWA MBUNGE WA TEMEKE MTOLEA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : CUF YAMJIA JUU ALIEKUWA MBUNGE WA TEMEKE MTOLEA.
kiungo : CUF YAMJIA JUU ALIEKUWA MBUNGE WA TEMEKE MTOLEA.

soma pia


CUF YAMJIA JUU ALIEKUWA MBUNGE WA TEMEKE MTOLEA.

Chama cha Wananchi (CUF) kimepokea Taarifa na sababu za aliekua Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea za kujivua Uanachama wake na kuomba vyana vinavyoona kua anaweza kushirikiana nae  na kutoa wito kua yupo tayari kwa mjadala na Vyama hivyo.

Kimsingi sabau zilizotolewa na Mtolea ni dhaifu na wala hazina ukweli wa aina yoyote.
 1 . Mbunge kukosa ushirikiano wa Chama chake si jambo linaloweza kukwamisha utekelezaji wa majukumu yake katika Jimbo na hasa ukizingatia kua Mbunge akishachaguliwa na kuapishwa basi anapaswa kuwatumikia wakaazi /Wananchi wote wa Jimbo lake na kamwe hapaswi kufanyakazi kwa kutumia tu Wanachama wa Chama Chake.

 Kwa hivyo kusema kua zaidi ya Miaka miwili amekosa ushirikiano wa Mtandao wa Chama chake katika kutekeleza Majukumu yake hii si sababu sahihi hata kidogo.

2. CUF-Chama cha Wananchi hakina mpango wala hakijaitisha Kamati ya Nidhamu na Maadili kwa lengo la kumjadili Mwanachama yoyote Yule si wiki ijayo wa mwezi ujao  kama alivyosikika akisema pale Bungeni kua sababu ya pili ya kujivua uanachama ni kwamba amepata taarifa kua wiki ijayo CUF imepanga kumfukuza.

Sababu hii nayo haina ukweli wowote kwakua Mtolea na Katani ni kati ya Wabunge waliokaribishwa kushiriki kwenye Kampeni za Jimbo la LIwale na walishiriki Kampeni hizo tangu Tarehe 02/10/2018 mpaka Tarehe 04/10/2018 waliporejea kwenye Majimbo yao.

Kama CUF ingekua na dhamira ya kumfukuza basi ingefanya hivyo pale alipojipa jukumu la kutafuta maharamia toka wa kuja kuvamia Ofisi Kuu Buguruni Jijini Dar es Salaam kwa kisingizio cha kufanya usafi.

Mtakumbuka kua alitumia nguvu kubwa kwa Vyombo vya habari kutangaza tukio hilo japo halikufanikiwa kwani Vijana wetu wa ulinzi walifanikiwa kuzima jaribio hilo.
3 . Mtolea alitoa wito kwa Chama chochote chenye Wabunge kama kinaona kinaweza kufanya nae kazi basi yupo tayari kufanya nao mazungumzo kwakua paomoja na kwamba anajiuzulu lakini bado anadhamira ya kuendelea kuwatumikia wakazi wa eti jimbo lake.

Hapana napo panatia mashaka , yani sio kwamba yeye Mtolea atafute Chama ambacho ataona kina sera,falsa,misingi na itikadi bora ili iwe rahisi kwake kuwatumikia Wanatemeke.

Lakini cha ajabu ndani ya Masaa 6 tayari Mtolea anaonekana kwenye Mitandao akiwa na Katibu Mkuu wa CCM na akiwa na Jezi ya CCM kuashiria kua Usajili umeshafanyika.

CUF-Chama cha Wananchi kinapenda kuujulisha UMMA kua kilichopelekea Mtolea kujivua Uanachama wake ni Usajili mpya uliotangzwa kua ungeishia jana na kwamba yoyote ataefanya usajili baada ya hapo hatapata fursa kama walizopata wale waliofanya usajili kabla ya Tarehe 15/11/2018.

Usajili wa sasa umeongeza chachu kubwa na kila anaetoka sasa kwa sifa hiyo ya Mbunge lengo kubwa la kua Waitara.

Thamani ya usajili hivi sasa kwa Wabunge sio tu kurejea kwenye nafasi yako bali pi nawe unaweza kubahatika kuupata Uwaitara . Kimsing wanaojiondoa hivi sasa ni wale wenye fikra na dhana hiyo.

KUHUSU SUALA LA KOROSHO
CUF-Chama cha Wananchi pamoja na kuipongeza Serikali katika kuikia lengo la kuhakikisha kua ina timiza lengo la kua Wakulima wa Korosho sio tu wanauza Korosho zao bali pia kuhakikisha kua wanauza kwa bei nzuri.

 Mjadala huu wa Zao la Korosho ulichukua akili za Watanzania wengi na kupelekea Rais kufanya Vikao na Wafanyabiashara kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wa sakata hilo na hatimae Serikali kuamua kununua Zao hilo.

Kama nilivyosema awali kua Cuf tunaungana na wadau wengine waliopongeza hatu hiyo muhimu ya utatuzi wa utata huo kwa msimu huu.

 Kama mnavyofahamu kua asilimia 90 ya Watanzania ni Wakulima na kilimo ni nyenzo muhimu ya uanzishaji wa Viwanda kwakua kilimo kinachangia asilimia 90 ya Malighafi za Viwandani kwa hivyo ni vyema kuwekeza kwenye kilimo kwa maana ya kunyanyua morali ya wakulima kwa kuwatafutia masoko ya Mazo yao yenye bei nzuri.

CUF-Chama cha Wanachi kinamtaka Waziri Mteule wa Kilimo kwa mashirikiano na Bodi ya Korosho kuweka Mkakati endelevu wa soko la Korosho kwakua si rahisi wa Serikali kua ndio itakua mnunuzi wa Korosho kila utapofika msimu wa Korosho.

 Mambo ya kilanguzi ya kangomba na Kula maua ndio yanayosababisha kushuka kwa bei kwakua Mkulima hana uwezo wa kupanga bei kutokana na ukweli kwamba tayari anadaiwa na Walanguzi.

CUF –Chama Cha Wananachi kinatoa wito kwa Serikali pia kutazama changamoto kama hizo ambazo pia zipo kwenye Mazo kama ya Pamba,Kahawa,Alizeti,Ufuta,Karafuu na mazao mengine ili kujinga taswira  sawia ya utatuzi  kwa Wakulima wote Nchini.

Bodi zetu za Mazao mbalimbali zijikite sio tu kwenye usimamizi wa uzalishaji kwa maana ya kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo bali pia ziwe na uwezo wa utafutaji wa Masoko ya Mazao yetu.

Nchi yetu ikifanikiwa kukuza kipato cha Mkulima basi itakua imefanikiwa kukuza kipato cha Mtanzania na hapo tutakua tumeanza harakati za kuimarisha sekta nyingine kama vile elimu,afya,Miundombinu na hata kukuza Sekta Binafsi.

Hata hivyo CUF –Chama Cha Wananchi kinafahamu kua katika utekelezaji wa agizo la Rais kutakuwepo Changamoto kama vile Wafanyabiashara wa Magodaoni na wale wenye Magari ya Usafirishaji na hata Wabebaji  wa Korosho kupakia kwenye Magari na Halmashauri kupoteza tozo za Ushuru na mambo mengine yanayofanana na hayo  laini hapa hoja muhimu ilozusha mjadala ni maslahi ya Mkulima wala haikua maslahi ya Makundi tajwa hapo juu na Maslahi ya Mkulima yamezingatiwa katika uwamuzi huu.



Hivyo makala CUF YAMJIA JUU ALIEKUWA MBUNGE WA TEMEKE MTOLEA.

yaani makala yote CUF YAMJIA JUU ALIEKUWA MBUNGE WA TEMEKE MTOLEA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala CUF YAMJIA JUU ALIEKUWA MBUNGE WA TEMEKE MTOLEA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/cuf-yamjia-juu-aliekuwa-mbunge-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "CUF YAMJIA JUU ALIEKUWA MBUNGE WA TEMEKE MTOLEA."

Post a Comment