title : HESLB YAKUTANA NA WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA WA CHUO CHA DUCE
kiungo : HESLB YAKUTANA NA WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA WA CHUO CHA DUCE
HESLB YAKUTANA NA WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA WA CHUO CHA DUCE
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) imekutana na wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) kwa ajili ya kutoa elimu kuhusiana na utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
Akizungumza na wanafunzi hao katika chuo hicho Meneja wa Upangaji Mikopo wa Bodi hiyo Julitha Miyedu amesema kuwa taratibu za kuomba mikopo ziko wazi na jinsi ya kuupata mkopo huo kutokana na vigezo na masharti vilivyoanishwa.Amesema kuwa Bodi ya Mikopo iko kwa ajili ya wanafunzi katika kuhakikisha kila mwenye vigezo vya mikopo anapata kwa wakati ili kuwezesha wanafunzi wasifikirie suala fedha katika kufanya mahitaji.
Miyedu elimu wanayoitoa kuhusiana na mikopo ni endelevu katika kuhakikisha kila mwanafunzi anapata uelewa wa bodi inavyochakata mikopo kwa wanafunzi.“Hatutamuacha mtu kwenye suala linalohusiana na utoaji mikopo nia ya bodi ni kuona kila mtu anapata mkopo kutokana vigezo vilivyoanishwa katika kuijenga nchi yetu na kupata watalaam mbalimbali”amesema Miyedu.
Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo Veneranda Malima amesema kuwa wanafunzi wanatakiwa kusoma vitu katika mitandao na vipeperushi vya bodi kwa kupata taarifa kufika ofisi za bodi kwa vitu vikubwa.Amesema kuwa bodi imeweka mfumo wa Kielekroniki katika kurahisisha malipo ya mikopo kwa wanafunzi kupitia kwa maafisa wa mikopo wa chuo.
Malima amesema kuwa Bodi itaendelea kutoa taarifa katika utaratibu uliozoeleka hivyo wanafunzi wajiepushe na kupata taarifa katika sehemu zisizo rasmi.
Meneja wa Upangaji Mikopo wa Bodi hiyo Julitha Miyedu akizungumza na wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) kuhusiana na ujio bodi katika utoaji wa mikopo ya elimu juu , iliyofanyika katika ukumbi wa chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Veneranda Malima akizungumza na wanfunzi wa mwaka wa kwanza wa DUCE.
Afisa Mikopo wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) Salmon Daud akitoa maelezo kwa wanafunzi wa chuo hicho kuhusiana na utaratibu wa kupata mikopo ni mara baada ya kujiridhisha na taarifa.
Baadhi ya Wanafunzi wa mwaka wa kwanza
Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Veneranda Malima akizungumza na wanfunzi wa mwaka wa kwanza wa DUCE.
Afisa Mikopo wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) Salmon Daud akitoa maelezo kwa wanafunzi wa chuo hicho kuhusiana na utaratibu wa kupata mikopo ni mara baada ya kujiridhisha na taarifa.
Baadhi ya Wanafunzi wa mwaka wa kwanza
Hivyo makala HESLB YAKUTANA NA WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA WA CHUO CHA DUCE
yaani makala yote HESLB YAKUTANA NA WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA WA CHUO CHA DUCE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HESLB YAKUTANA NA WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA WA CHUO CHA DUCE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/heslb-yakutana-na-wanafunzi-wa-mwaka-wa.html
0 Response to "HESLB YAKUTANA NA WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA WA CHUO CHA DUCE"
Post a Comment