title : DODOMA ITAKAVYOKUWA USIPIME....JIJI LAKE KUFANANISHA NA MIJI YA MAJUU SIO LA DAR
kiungo : DODOMA ITAKAVYOKUWA USIPIME....JIJI LAKE KUFANANISHA NA MIJI YA MAJUU SIO LA DAR
DODOMA ITAKAVYOKUWA USIPIME....JIJI LAKE KUFANANISHA NA MIJI YA MAJUU SIO LA DAR
*Aeleza jinsi tamko la Rais lilivyoleta mabadiliko makubwa
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.
WAKATI Rais Dk.John Magufuli akitarajiwa kuhamia rasmi katika Jiji la Dodoma Desemba mwaka huu, tayari mikakati mbalimbali inaendelea la kuliweka sawa Jiji hilo kuhakikisha linaendana na hadhi ya kuwa makao makuu ya Serikali.
Kwa sasa kuna miradi mbalimbali ya ujenzi wa maendeleo inayoendelea kufanyika kwa kasi kubwa kuhakikisha Jiji la Dodoma linapendeza na kuwa na muonekano wa aina yake ambapo Mkurugenzi wa Jiji hilo Godwin Kunambi ameeleza hatua kwa hatua namna ambavyo wamejipanga.
Akizungumza na Michuzi Blog na Michuzi TV kwenye mahojiano maalumu yaliyofanyika Mjini Dodoma Kunambi amesema kuwa baada ya Rais Dk.John Magufuli kutangaza Dodoma kuwa Jiji na Serikali kuhamia rasmi kuna hatua mbalimbali zimechukuliwa.
"Kuna mambo makubwa ambayo Rais wetu mpendwa ameyafanya baada ya kutangaza Dodoma kuwa Jiji na kuhamishiwa kwa shughuli za Serikali Kuu.Tunakumbuka aliamua kuivunja CDA na shughuli za CDA kuhamishiwa Manispaa ya Dodoma na baadae kuwa Jiji.Niwahakikishie Watanzania baada ya tamko la Rais la kuhamishia Serikali Dodoma kuna mambo makubwa yamefanyika,"amesema.
Amefafanua baada ya tamko hilo, Jiji la Dodoma nalo likaanza kuweka mikakati yake kufanikisha dhamira ya Rais ambapo moja ya mambo ambayo walifanya ni kuandika maandiko kwa ajili ya kupata fedha za kwa ajili ya miradi mitano waliyoamua kuanza nayo katika kuboresha Jiji hilo.
"Maandiko yetu yalisaidia kupata fedha kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa kituo kikubwa cha mabasi ambacho tunaamini kitakuwa cha kwanza kwa ukubwa Afrika Mashariki, soko la kisasa , maeneo ya kupumzika, ujenzi wa miundombinu ya barabara, dampo la kisasa la kuhifadhi taka na eneo la kuegesha malori,"amesema Kunambi.
Hivyo makala DODOMA ITAKAVYOKUWA USIPIME....JIJI LAKE KUFANANISHA NA MIJI YA MAJUU SIO LA DAR
yaani makala yote DODOMA ITAKAVYOKUWA USIPIME....JIJI LAKE KUFANANISHA NA MIJI YA MAJUU SIO LA DAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DODOMA ITAKAVYOKUWA USIPIME....JIJI LAKE KUFANANISHA NA MIJI YA MAJUU SIO LA DAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/dodoma-itakavyokuwa-usipimejiji-lake.html
0 Response to "DODOMA ITAKAVYOKUWA USIPIME....JIJI LAKE KUFANANISHA NA MIJI YA MAJUU SIO LA DAR"
Post a Comment