title : Diwani Neema wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala atembelea Yatima
kiungo : Diwani Neema wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala atembelea Yatima
Diwani Neema wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala atembelea Yatima
Diwani wa viti Maalum Manispaa ya Ilala Neema Nyangalilo akiwa na viongozi wa Umoja wa Wanawake UWT kata ya Ilala wakati walipokwenda kutembelea watoto yatima wa kituo cha msimbazi
Picha na Heri Shaaban
Na Heri Shaaban
Mwambawahabari
DIWANI wa Viti Maalum Wanawake Manispaa ya Ilala Neema Nyangalilo amesherekea miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Magufuli kwa kugawa vyakula katika kituo cha watoto Yatima Msimbazi wilayani Ilala.
"Mimi kama Diwani wa Viti Maalum Wanawake Manispaa ya Ilala nimpongeza Rais wangu Magufuli katika uongozi wake pia nimetumia siku ya leo kushiriki katika kituo cha Msimbazi kuwaona watoto na kuwapa misaada"alisema Neema.
Neema alisema msafara wake alikuwa na UWT pamoja na viongozi wake waliweza kujifunza jambo kama wazazi mara b aada kuona watoto waliotelekezwa na walioachwa na wazazi wao kutokana na sababu mbalimbali ikiwepo uzazi.
Aliitaka wananchi wawe wanatenga muda ama siku katika kutembelea kituo cha watoto yatima.
Wakati huo Diwani Neema alisema kwa sasa mikakati yake ambayo amejiwekea ni kusaidia utoaji elimu kwa vikundi vya Wanawake wa Manispaa ya Ilala ili waweze kupata elimu ya kutosha waandae katiba za vikundi vyao wapate mikopo ya Manispaa kupitia Dar es Salaam Benki (DCB).
Alisema yeye kama Diwani anasimamia utekelezaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM)pamoja na madiwani wa manispaa ya Ilala kuakikisha Wanawake wote ambao wamesajili Vikundi kupitia Manispaa pesa wanapata mikopo hiyo hisio na riba .
Alisema kwa sasa mwamko wa wanawake mkubwa katika kujikwamua kiuchumi na wengi wengi wamejingiza katika kujishughulisha katika biashara mbalimbali wameacha maisha tegemezi .
Kwa upande wake Msaidizi Kiongozi wa kulea Watoto yatima wa Kituo cha Msimbazi Sisita Maria Ettiene alisema kituo cha Msimbazi kwa sasa wapo watoto 36 wengi hawana mama wazazi wao walikufa kwa uzazi wengine wametelekezwa .
Maria alisema utaratibu wa kupokea watoto wanaletewa na Ustawi wa Jamii .
Hivyo makala Diwani Neema wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala atembelea Yatima
yaani makala yote Diwani Neema wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala atembelea Yatima Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Diwani Neema wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala atembelea Yatima mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/diwani-neema-wa-viti-maalum-manispaa-ya.html
0 Response to "Diwani Neema wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala atembelea Yatima"
Post a Comment