title : DC CHONGOLO AISHAURI CMPD KUANZISHA PROGRAM TUMISHI YA USAFIRI.
kiungo : DC CHONGOLO AISHAURI CMPD KUANZISHA PROGRAM TUMISHI YA USAFIRI.
DC CHONGOLO AISHAURI CMPD KUANZISHA PROGRAM TUMISHI YA USAFIRI.
Na John Luhende
Mwambawahabari
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni mhe. Daniel Chongolo amekishauri chama cha madereva na wamiliki wa Boda boda Mkoa wa Dar es salaam CMPD kuanzisha program tumishi ya usafiri watakayoitumia ilikuendesha kisasa biashara ya usafiri wa piki piki jijini hapa.
Chongolo ametoa ushauri huo wakati akizungumza na madereva na wamiliki wa Bodaboda Wilaya ya Kinondoni nakusema kuwa atahakikisha Manispaa inavitambua, kuvisajili na kuvisimamia vituo takribani 444, vilivyopo katika Kata na Mitaa ya Manispaa hiyo kwa kuzingatia,miongozo sheria, kanuni na taratibu ilikuongeza mapato ya serikali.
Erasto Lahi ni Mkurugenzi wa operesheni wa Kampuni ya TAMOBA inayojishugulisha na ulinzi na usalama iliyoingia makubaliano na chama cha madeva na wamiliki wa Pikipiki mkoa wa Dar es salaam CMPD kufunga vifaa vya kudhibiti wizi wa Boda boda GPS,amesema kampuni yao wanaweza kuuendesha mfumo huo na wanautaalamu wa kutosha .
Akitoa taarifa ya vituo hivyo vya bodaboda na bajaji, Mwenyekiti wao ndugu Festo Swai, amesema upo umoja wao uitwao CMPD, ulionzishwa kwa lengo la kusaidiana na kushughulikia changamoto zinazowakabili wao kama vikundi vidogo vidogo, zikiwemo kutosajiliwa na kutambuliwa, kutopatiwa mikopo ya vijana, kutozijua haki zao pindi wanapokutwa na kosa la barabarani, kuuwawa na kuporwa mali zao, pamoja na kupatiwa njia ya kusafirisha abiria mjini.
Akijibu swali linalomtaka bodaboda au bajaji kupelekwa mahabusu pindi afanyapo kosa kwa niaba ya OCD Kinondoni, Inspekta Serengeti amesema, dereva wa bajaji au bodaboda kufanya kazi zake bila kuwa na leseni na viambata vyote atakiwavyo kuwanavyo dereva , atashitakiwa kwa kosa la usalama barabarani.
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii anayehusika na Mikopo, Bi Florah Msilu, katika kufafanua suala la mikopo kwa vijana amesema, kwa mwaka wa fedha 2017/2018, Kinondoni imetenga takribani bilioni 2.7, kwa ajili ya mikopo, na kuwataka vijana wenye umri kuanzia miaka 18-35, katika vikundi kuchangamkia fursa hiyo.
.
Hivyo makala DC CHONGOLO AISHAURI CMPD KUANZISHA PROGRAM TUMISHI YA USAFIRI.
yaani makala yote DC CHONGOLO AISHAURI CMPD KUANZISHA PROGRAM TUMISHI YA USAFIRI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC CHONGOLO AISHAURI CMPD KUANZISHA PROGRAM TUMISHI YA USAFIRI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/dc-chongolo-aishauri-cmpd-kuanzisha.html
0 Response to "DC CHONGOLO AISHAURI CMPD KUANZISHA PROGRAM TUMISHI YA USAFIRI."
Post a Comment