title : CHINA DASHENG BANK LIMITED YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM, KUSAIDIA UCHUMI WA VIWANDA
kiungo : CHINA DASHENG BANK LIMITED YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM, KUSAIDIA UCHUMI WA VIWANDA
CHINA DASHENG BANK LIMITED YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM, KUSAIDIA UCHUMI WA VIWANDA
NA K-VIS BLOG
BENKI mpya ya China Dasheng Bank Limited, inaanza kutoa huduma leo Jumatatu Novemba 26, 2018, jijini Dar es Salaam, ikiwa na mtaji wa kuanzia wa dola za kimarekani milioni 40 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 92, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya benki hiyo Bw. Yu Jiaqin amesema.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa benki hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Bw. Yu Jiaqin amesema benki hiyo ni benki ya kibiashara inayomilikiwa na makampuni sita ya serikali ya China yakishirikiana na makampuni binafsi kutoka mji wa Shanghai na Jiangsu.
Benki hii inalenga kutoa huduma kwa makampuni makubwa ya kichina yanayofanya miradi mbalimbali hapa nchini, lakini pia watanzania wanaofanya biashara na China ikizingatia makundi yote ya watu wenye kipato cha chini, cha kati na cha juu, alisema Bw. Jiaqin.
“Tutatoa huduma za bidhaa zote za kawaida za kibenki kama vile akaunti za akiba, akaunti za kudumu na za muda maalum, mikopo ya muda mfupi na muda mrefu na mikopo hii itatolewa kwa shilingi za kitanzania pamoja na fedha za kigeni.” Alibainisha Mwenyekiti huyo wa bodi.
Aidha Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bi Nunu Saghaf alishukuru Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kutoa leseni ya kufanya biashara kwa benki yake na kuahidi kuisaidia serikali ya Tanzania katika kufikia malengo yake ya uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, akitoa hotuba yake.
Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Wang Ke akitoa hotuba yake.

Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa China Dasheng Banki Limited, Bi. Nunu Saghaf (watatu kushoto mstari wa mbele akiwa na wageni mbalimbali kwenye hafla hiyo ya uzinduzi.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
Hivyo makala CHINA DASHENG BANK LIMITED YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM, KUSAIDIA UCHUMI WA VIWANDA
yaani makala yote CHINA DASHENG BANK LIMITED YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM, KUSAIDIA UCHUMI WA VIWANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CHINA DASHENG BANK LIMITED YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM, KUSAIDIA UCHUMI WA VIWANDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/china-dasheng-bank-limited-yazinduliwa.html
0 Response to "CHINA DASHENG BANK LIMITED YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM, KUSAIDIA UCHUMI WA VIWANDA"
Post a Comment