title : BILIONI 50 ZATOLEWA KUKARABATI UWANJA WA NDEGE MTWARA
kiungo : BILIONI 50 ZATOLEWA KUKARABATI UWANJA WA NDEGE MTWARA
BILIONI 50 ZATOLEWA KUKARABATI UWANJA WA NDEGE MTWARA
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii ,Mtwara
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi inakarabati Uwanja wa ndege wa Mtwara kwa kiasi cha Sh bilioni 50 hili uweze kurahisisha huduma za usafiri wa anga.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisa Uendeshaji wa uwanja huo, Zitta Majinge amesema Ukarabati huo unahusisha ujenzi wa barabara ya kuingia uwanjani yenye urefu wa kilomita 1.2, maegesho ya ndege na njia za kurukia na kutua ndege.
Akizungumza jana, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, alisema ukarabati huo unafanywa na Kampuni ya Beijing Constraction Engineering Group ( BCEG)."ukarabati huo unafanywa na Kampuni ya Beijing Constraction Engineering Group (BCEG) kwa muda ya miezi 24. Mkandarasi yupo katika hatua za maandalizi na ujenzi wa kambi ya ofisi ya mhandisi mshauri,"amesema
Amesema mradi huo ulisainiwa Novemba 11 mwaka jana na kuanza rasmi Juni 26 mwaka huu na unatarajiwa kukamilika Septemba 2020.Naye Ofisa Uendeshaji wa uwanja huo, Zitta Majinge, alisema urefu wa njia ya kuruka na kutua ndege kwa sasa ni mita 2,258 na kutokana na ukarabati huo zitaongezwa mita 542 wakati upana utaongezeka kutoka mita 35 hadi 45.
Amesema ndege zenye uwezo wa kutua uwanjani hapo kwa sasa ni zile zenye uzito wa tani 70 na kwamba baada ya ukarabati huo wanatarajia zitatua ndege zenye uzito wa tani 300."Ukarabati ukikamilika kiwanja kitakuwa na uwezo wa kuhudumia ndege kubwa zaidi. Hivi sasa makampuni mengi yanaomba kuja lakini yanashindwa kutokana na miundombinu mingi kuchoka hasa njia za kurukia na kutua ndege," amesema Majinge.
Amesema changamoto nyingine ni kuwapo kwa pori kubwa ambalo wakati mwingine limekuwa na wanyama wakali na kusababisha utendaji kazi kuwa mgumu.Hata hivyo amesema wako kwenye hatua za kupunguza msitu huo ili waanze mchakato wa ujenzi wa uzio.Uwanja huo uliojengwa mwaka 1950 kwa mwaka unahudumia zaidi ya abiria 10,000.
Ofisa Uendeshaji wa uwanja wa Ndege wa Mtwara , Zitta Majinge akizungumza na Waandishi wa habari waliofika katika uwanja huo kuona upanuzi wa uwanja huo.
Ofisa Uendeshaji wa uwanja wa Ndege wa Mtwara , Zitta Majinge akifafanua jambo kwa Waandishi Wahabari
Sehemu ya jengo la Utawala la uwanja wa Ndege wa Mtwara
Hivyo makala BILIONI 50 ZATOLEWA KUKARABATI UWANJA WA NDEGE MTWARA
yaani makala yote BILIONI 50 ZATOLEWA KUKARABATI UWANJA WA NDEGE MTWARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BILIONI 50 ZATOLEWA KUKARABATI UWANJA WA NDEGE MTWARA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/bilioni-50-zatolewa-kukarabati-uwanja.html
0 Response to "BILIONI 50 ZATOLEWA KUKARABATI UWANJA WA NDEGE MTWARA"
Post a Comment