title : BALOZI ADADI AWAFUNDA VIJANA TAMASHA LA UTAMADUNI WA BONDE
kiungo : BALOZI ADADI AWAFUNDA VIJANA TAMASHA LA UTAMADUNI WA BONDE
BALOZI ADADI AWAFUNDA VIJANA TAMASHA LA UTAMADUNI WA BONDE
MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu amewataka vijana wilayani humo kuacha kuvaa suruali na kuzishusha chini maarufu kama milegezo, mini sketi kwani kufanya hivyo kunapelekea kuondoa utamaduni wa kitanzania hususani za watu wa bonde kupotea badala yake wavae nguo za asili zenye heshima.
Kwani uvaaji huo wa nguo unapelekea kupoteza mila na tamaduni ambao uliopo huku akiwataka kubadilika kwa kuhakikisha wanavaa mavazi asili ambayo ni desturi kwa watanzania.
Hayo yalisemwa na Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu wakati wa Tamasha la Bonde ambalo lilifanyika Kata ya Kicheba wilayani Muheza lililokwenda sambamba na maonyesho ya vitu mbalimbali vya asili ikiwemo vyakula.
“Tamasha la Bonde linapaswa tuliendeleze kwa vizazi vya sasa na vijavyo waweze kujua tamaduni na mila zao ,lakini pia mambo ya mavazi badala ya kuvaa milegezo, mini sketi huku mavazi na desturi zetu vinapotea tuvae nguo za asili zenye heshima kwani bila kufanya hivyo mavazi na desturi vitapotea”Alisema Mbunge huyo .Mbunge huyo alisema pia ni muhimu tamaduni za kibondei kuhakikisha zinaendelezwa kila mwaka kupitia tamasha hilo kwa kuyafadili ili vijazi vya sasa na vijavyo viweze kujua mila zao huku akiwasisitiza wazee waliopo kutokuondoka nazo maana vijana wanaozaliwa wanaweza kuona mambo hayo hayawezekani.
Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto akiwa na Zumbe wa Kitulwe Tibua Charles Nkuninga kulia wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye Tamasha la Bonde ambalo lilifanyika Kata ya Kicheba wilayani Muheza lililokwenda sambamba na maonyesho ya vitu mbalimbali vya asili ikiwemo vyakula
Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akizungumza wakati wa Tamasha hilo
Afisa Utamaduni wa wilaya ya Muheza Msafiri Charles Nyaluka akizungumza katika Tamasha hilo
Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto akitazama bidhaa mbalimbali vinavyotengenezwa na wakima mama wa Kibondei wakati alipotembelea Maonyesho hayo wakati Tamasha la Bonde lililofanyika eneo la Kicheba wilayani Muheza
MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kulia akilakiwa na wananchi wa Kijiji Kicheba Kata ya Kicheba wilayani Muheza wakati alipokwenda kwenye Tamasha la Bonde.
Hivyo makala BALOZI ADADI AWAFUNDA VIJANA TAMASHA LA UTAMADUNI WA BONDE
yaani makala yote BALOZI ADADI AWAFUNDA VIJANA TAMASHA LA UTAMADUNI WA BONDE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BALOZI ADADI AWAFUNDA VIJANA TAMASHA LA UTAMADUNI WA BONDE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/balozi-adadi-awafunda-vijana-tamasha-la.html
0 Response to "BALOZI ADADI AWAFUNDA VIJANA TAMASHA LA UTAMADUNI WA BONDE"
Post a Comment