title : ATHMANI AENDELEA KUOMBA MSAADA WA MATIBABU KWA WATANZANIA
kiungo : ATHMANI AENDELEA KUOMBA MSAADA WA MATIBABU KWA WATANZANIA
ATHMANI AENDELEA KUOMBA MSAADA WA MATIBABU KWA WATANZANIA
NA YEREMIAS NGERANGERA,NAMTUMBO
Athmani Amani mkazi wa kijiji cha Naikesi kata ya kitanda wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma anawaomba watanzania kumsaidia fedha za kugharimia matibabu ya mtoto wake Shaziri Athmani (12) anayesumbuliwa na tatizo la moyo kuwa mkubwa.
Mtoto Shaziri Athamani ni mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Naikesi iliyopo kata ya Kitanda wilayani Namtumbo awali alikuwa anasumbuliwa na kuvimba miguu hali iliyokuwa inamkosesha masomo yake darasani mara kwa mara kuanzia mwaka 2016.
Mwaka huo huo mwezi septemba baba yake alilazimika kumpeleka Hospitali ya Mkoa Songea kuangalia tatizo la kuvimba kwa miguu ya mtoto huyo na baada ya kupata vipimo wakashauriwa kuenda Hospitali ya Peramiho .
Bwana Athamani alidai kuwa hakuwa na fedha za kumpeleka mtoto peramiho kwa kipindi hicho na badala yake alirudi naye nyumbani Naikesi kwenda kuuza mifugo lakini fedha hizo hazikumwezesha kukidhi mahitaji ya kumtibu mwanae katika Hospitali ya Peramiho baada ya kufika katika Hospitali hiyo na kumaliza fedha yake yote aliyokuwa nayo katika vipimo pekee .
Baada ya kupatiwa vipimo na kubaini Tatizo la mwanae alirudi na mwanae mpaka kijijini kwake kujipanga upya kwa ajili ya matibabu ya mwanae na kujitahidi kwa kile anachokipata anunue dawa kwa ajili ya mwanae huyo.
Pamoja na jitihada hizo hali ikaendelea kuwa sio nzuri na ndipo alipolazimika kufanya kazi za kulima mashamba ya watu ili apate fedha za kumtibu kijana wake na mwaka huu mwezi oktoba alimpeleka kijana wake huyo peramiho na baada ya kufika peramiho na kupatiwa vipimo alishauriwa na madaktari kumpeleka mtoto huyo Hospitali ya Muhimbili Dar es salaam.
Hata hivyo mzazi huyo aliomba msaada vyombo vya habari kumsaidia tatizo lake ili aweze kuchangiwa na wasamaria wema ampeleke mtoto wake muhimbili ambapo vyombo vya habari vilimsaidia na aliweza kusaidiwa michango iliyomwezesha kumfikisha kijana wake muhimbili na kupatiwa matibabu ya awali.
Anawashukuru Watanzania wote waliomchangia kijana wake na kuweza kupata matibabu ya awali lakini anawaomba waendelee kumchangia kwani kila baada ya miezi mitatu anatakiwa kumpeleka kijana wake huyo hospitalini hapo na yeye hana uwezo wa wa fedha za kumpeleka hospitali kijana wake huyo mara kwa mara muhimbili zaidi ya kuwategemea wasamaria wema .
Kijana huyo baada ya kupata matibabu ya awali ameanza kuonesha hali ya matumaini tofauti na ilivyoawali kabla ya kumpeleka Muhimbili kwa matibabu ya awali alisema mzazi huyo.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj67KHKSPponLqBSw4kmWKg_083cbCsxtResK29geW7JWj8PuRfA9S3-Rc2sLJw9JSySfDUiD0oISocLatukLV7QF7vP19re7imstpFmGZQchZ3eXutWdjojIIhTkQ_IAgusdrowcl2_QOb/s640/IMG_20171027_121121.jpg)
Athmani Amani mkazi wa kijiji cha Naikesi kata ya kitanda wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma anawaomba watanzania kumsaidia fedha za kugharimia matibabu ya mtoto wake Shaziri Athmani (12) anayesumbuliwa na tatizo la moyo kuwa mkubwa.
Hivyo makala ATHMANI AENDELEA KUOMBA MSAADA WA MATIBABU KWA WATANZANIA
yaani makala yote ATHMANI AENDELEA KUOMBA MSAADA WA MATIBABU KWA WATANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ATHMANI AENDELEA KUOMBA MSAADA WA MATIBABU KWA WATANZANIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/athmani-aendelea-kuomba-msaada-wa.html
0 Response to "ATHMANI AENDELEA KUOMBA MSAADA WA MATIBABU KWA WATANZANIA"
Post a Comment