ZAIDI YA WATU 300 WAFANYIWA UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO KIGAMBONI

ZAIDI YA WATU 300 WAFANYIWA UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO KIGAMBONI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ZAIDI YA WATU 300 WAFANYIWA UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO KIGAMBONI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ZAIDI YA WATU 300 WAFANYIWA UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO KIGAMBONI
kiungo : ZAIDI YA WATU 300 WAFANYIWA UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO KIGAMBONI

soma pia


ZAIDI YA WATU 300 WAFANYIWA UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO KIGAMBONI

Na Genofeva Matemu – JKCI

1/10/2018 Zaidi ya watu 300 wamefanyiwa upimaji wa magonjwa ya moyo pamoja na kupewa elimu ya lishe bora kwa afya ya moyo katika maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Hospitali ya Vijibweni iliyopo wilaya ya Kigamboni.

Katika upimaji huo uliofanywa na madaktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari wa Moyo Tanzania (THF) jumla ya watu 169 wakiwemo watoto walipimwa kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO Cardiogram ECHO) na 135 ambao ni watu wazima walipima kipimo cha kuangalia jinsi umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiography-ECG).

Akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Samweli Rweyemamu alisema kwa upande wa watoto waliwaona 34 sita kati yao walikutwa na matatizo ya moyo na watu wazima 10 walikutwa na matatizo wote hao wamepewa rufaa ya moja kwa moja ya kwenda kutibiwa JKCI.

“Wananchi wengi tuliowaona na kuwafanyia vipimo wamekutwa na tatizo la shinikizo la juu la damu ambapo tumewapa dawa za kwenda kutumia pamoja na ushauri na wachache kati yao tumewapa dawa za ugonjwa wa kisukari”, alisema Dkt. Rweyemamu.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Smitha Bhalia akitoa maelekezo ya jinsi ya kutumia dawa kwa mkazi wa Kigamboni wakati wa maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani ambapo Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari wa Moyo Tanzania (THF) walifanya upimaji bila malipo katika viwanja vya Hospitali ya Vijibweni iliyopo wilaya ya Kigamboni. Katika upimaji huo makampuni mbalimbali ya dawa za binadamu yaligawa dawa bure kwa watu waliokutwa na matatizo yaliyohitaji kutumia dawa.



Hivyo makala ZAIDI YA WATU 300 WAFANYIWA UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO KIGAMBONI

yaani makala yote ZAIDI YA WATU 300 WAFANYIWA UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO KIGAMBONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ZAIDI YA WATU 300 WAFANYIWA UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO KIGAMBONI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/zaidi-ya-watu-300-wafanyiwa-upimaji-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "ZAIDI YA WATU 300 WAFANYIWA UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO KIGAMBONI"

Post a Comment