title : WAZIRI MKUU AITAKA SIDO KUBUNI TEKNOLOJIA RAFIKI
kiungo : WAZIRI MKUU AITAKA SIDO KUBUNI TEKNOLOJIA RAFIKI
WAZIRI MKUU AITAKA SIDO KUBUNI TEKNOLOJIA RAFIKI
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameliagiza Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO)lijielekezekatika kubuni teknolojia na mitambo rafiki inayolenga kutatua changamoto za wajasiriamali kulingana na mazingira yao.
Amesema Serikali inaendelea kuimarisha shughuli za SIDO lakini bado kuna changamoto za wajasiriamali wadogo ambazo lazima zishughulikiwe kwa kasi kubwa ili kufungamanisha shughuli za SIDO na uchumi wa Viwanda
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Oktoba 23, 2018) wakati akifungua Maonesho ya SIDO kitaifa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Nyakabindi vilivyoko wilayani Bariadi mkoani Simiyu na kuhudhuriwa na wajasiriamali 500.
Amesema ili kufikia uchumi wa kati inambidi kila Mtanzania mahali alipo afanye kazi kwa bidii, maarifa na ubunifu. “Tusipoteze wakati kwa kufanya mambo yasiyo na tija. Tuzingatie falsafa ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Hapa Kazi Tu.”
“Mfano kwa hapa Bariadi, tunatarajia SIDO watuletee teknolojia na mitambo inayoweza kurahisisha ukamuaji wa mafuta yanayotokana na mbegu za alizeti na pamba, kwa Dodoma taknolojia na mitambo kwa ajili ya kuchakata zabibu.”
“Kigoma pelekeni teknolojia na mitambo kwa ajili ya kuchakata mbegu za michikichi na kwenye maeneo yanayolimwa korosho teknolojia na mitambo ya kubangua korosho na maeneo kama Ilula ambayo yanazalisha nyanya kwa wingi wapate teknolojia na mitambo ya kusindika na kuhifadhi nyanya na mbogamboga.”
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Maonesho ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, Oktoba 23, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Badhi ya wananchi wa mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kufungua Maonesho ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kwenye uwanja wa Nyakabindi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) kitanzania ili wakue na kuwa wawekezaji wakubwa. Pia kuwawekea mazingira wezeshi ya kufanya shughuli zao.”
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chaki zilizotengenezwa wilayani Maswa katika maonesho ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, Oktoba 23, 2018
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea jembe la asili kutoka mhunzi, Mashaka Daniel wa Bukoba katika Maonesho ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) aliyoyafungua kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, Oktoba 23, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa Ufundi wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Prosper Godfrey (kulia) kuhusu majiko makubwa yanayotengenezwa na SIDO wakati alipofungua Maonesho ya SIDO kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu Oktoba 23, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simyu, Anthony Mtaka na watatu kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya.
Hivyo makala WAZIRI MKUU AITAKA SIDO KUBUNI TEKNOLOJIA RAFIKI
yaani makala yote WAZIRI MKUU AITAKA SIDO KUBUNI TEKNOLOJIA RAFIKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AITAKA SIDO KUBUNI TEKNOLOJIA RAFIKI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/waziri-mkuu-aitaka-sido-kubuni.html
0 Response to "WAZIRI MKUU AITAKA SIDO KUBUNI TEKNOLOJIA RAFIKI"
Post a Comment