title : WASANII WA FILAMU RAY, DUDE WACHANGAMKIA FURSA APP YA MP TV
kiungo : WASANII WA FILAMU RAY, DUDE WACHANGAMKIA FURSA APP YA MP TV
WASANII WA FILAMU RAY, DUDE WACHANGAMKIA FURSA APP YA MP TV
Kutoka kushoto ni Balozi wa MP Tv hapa nchini Jocob Stephen ‘JB’, Afisa Mipango wa App ya MP Tv nchini Msanii Daudi Michael ‘Duma’ pamoja Msanii mkongwe wa filamu nchini, Vicent Kigosi 'Ray' wakizumgumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Waigizaji wa filamu za kibongo Vicent Kigosi 'Ray' pamoja na Kulwa Kikumbe 'Dude' wameipongeza App ya MP Tv kwa kuendelea kuwa msaada hapa nchini kwa kununua kazi za filamu kwa makubaliano rafiki.
MP Tv inampa fursa mtazamaji wa filamu kuangalia filamu mbalimbali za ndani na nje ya nchi gharama nafuu ya Sh I,I99 kwa wiki.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Msanii mkongwe wa filamu nchini, Vicent Kigosi 'Ray' amesema kuwa App ya MP Tv imekuwa msaada kutokana awali wahindi walikuwa wanawanyonya kiuchumi.
Ray amesema kuwa kutokana ujio wa MP Tv kuanzia leo filamu aliyoicheza 'IMETOSHA' itakuwa inaonekana kupitia MP Tv baada ya mtazamaji kulipia Sh I,999.
Amesema kuwa hii ni fursa kwa wapenzi wa filamu kuangalia filamu mbalimbali wanazozipenda kwa gharama nafuu tofauti na awali.
"Tunaishukuru sana MP Tv kutokana imekuja kuiokoa tasnia ya filamu hapa nchin, na filamu ya Imetosha ni nzuri na watazamaji wataendelea kuangalia kupitia MP Tv" amesema Ray.
Kulwa Kikumbe 'Dude' amesema kuwa kutokana na uwepo wa MP Tv hapa nchini filamu yake ya Bongo Dar es Salaam itakuwa inapatika katika MP TV.
Dude amesema kuwa filamu ya bongo Dar es Salaam ni filamu nzuri ambayo imelenga kuelimisha umma kuhusu matapeli wanavyotumia mbinu mpya kutapeli watu.
Dude amesema kuwa ni vizuri watanzania wakaangalia filamu hiyo katika MP Tv ili kuepukana na mbinu za matapeli hapa nchini.
Afisa Mipango wa App ya MP Tv nchini Msanii Daudi Michael ‘Duma’ amesema kuwa kutangazwa kwa filamu hizo ni mwendeleo wa App hiyo kwa kila mwezi kutangaza filamu mpya ambazo zitakuwa zimenunuliwa kwa ajili ya kuoneshwa na MP Tv.
Balozi wa MP Tv hapa nchini Jocob Stephen ‘JB’, amesema kuwa MP TV ni fursa kwa wazalishaji wa filamu haoa nchini kutangaza filamu zao ili zifahamike kimataifa.
JB amesema kuwa wazalishaji wa filamu wakati umefika kutumia fursa hiyo kuwa kuandaa kazi kwa ajili ya kuonekana kupitia App ya MP Tv na kujitangaza nchi mbalimbali.
MP TV imeendelea kuleta ahueni katika tasnia ya filamu hapa nchini baada ya kuendelea kununua filamu za kibongo zinazofanya vizuri kwa makubaliano maalum.
Makubaliano hayo ni rafiki kwa msanii mwenye kazi husika kutokana MP Tv imekuwa ikinunua kwa muda maalum kulingana maelewana na muhusika.
Uwepo wa MP Tv hapa nchini ni chachu ya mafanikio katika tasnia ya filamu hapa nchini kutoka awali wasanii walikuwa wanapata kipato kidogo tofauti na kazi zao.
Hivyo makala WASANII WA FILAMU RAY, DUDE WACHANGAMKIA FURSA APP YA MP TV
yaani makala yote WASANII WA FILAMU RAY, DUDE WACHANGAMKIA FURSA APP YA MP TV Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WASANII WA FILAMU RAY, DUDE WACHANGAMKIA FURSA APP YA MP TV mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/wasanii-wa-filamu-ray-dude-wachangamkia.html
0 Response to "WASANII WA FILAMU RAY, DUDE WACHANGAMKIA FURSA APP YA MP TV"
Post a Comment