WALIOZEMBEA KUSIMAMIA,KUJENGA MRADI WA MAJI UKALAWA-KITOLE, MKOANI NJOMBE WATAKIWA KUISAIDIA POLISI

WALIOZEMBEA KUSIMAMIA,KUJENGA MRADI WA MAJI UKALAWA-KITOLE, MKOANI NJOMBE WATAKIWA KUISAIDIA POLISI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WALIOZEMBEA KUSIMAMIA,KUJENGA MRADI WA MAJI UKALAWA-KITOLE, MKOANI NJOMBE WATAKIWA KUISAIDIA POLISI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WALIOZEMBEA KUSIMAMIA,KUJENGA MRADI WA MAJI UKALAWA-KITOLE, MKOANI NJOMBE WATAKIWA KUISAIDIA POLISI
kiungo : WALIOZEMBEA KUSIMAMIA,KUJENGA MRADI WA MAJI UKALAWA-KITOLE, MKOANI NJOMBE WATAKIWA KUISAIDIA POLISI

soma pia


WALIOZEMBEA KUSIMAMIA,KUJENGA MRADI WA MAJI UKALAWA-KITOLE, MKOANI NJOMBE WATAKIWA KUISAIDIA POLISI

Kutokua makini katika uratibu, usimamizi na ujenzi wa mradi wa maji mkoani Njombe kumewaweka matatani baadhi ya watendaji wa serikali na wakandarasi waliopewa dhamana ya kujenga na kufikisha majisafi na salama kwa wananchi.

Mradi uliotiliwa shaka wa Ukalawa na Kitole umesubiriwa na wananchi kwa zaidi ya miaka mitano na bado umekua butu kukidhi kiu ya wakazi wa vijiji vya Ukalawa na Kitole. Mradi huo umejengwa na kampuni ya Kihanga Farm International iliyolipwa kiasi cha Shilingi Milioni 532 kati ya Shilingi Milioni 562.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameelekeza wahusika walioshiriki katika mradi huo wakiwamo Watalaam wa maji wa Serikali popote walipo, Mhandisi Mshauri wa mradi na Mkandarasi wa mradi wasaidie Jeshi la Polisi kupata undani wa taarifa zinazohusu mradi, ikiwamo malipo yaliyofanyika wakati wananchi hawapati maji.

Mhe. Aweso (Mb) katika kikao kilichodumu kwa saa sita kilichowakutanisha watalaam wa maji, na baadhi ya walioshiriki katika ujenzi wa mradi wa maji Ukalawa-Kitole, amesema miradi ya maji sio kichaka cha kupitisha fedha na kusisitiza endapo mhusika yoyote atabainika kushiriki kuhujumu mradi huo, hata kama amestaafu utumishi wa umma, atatafutwa popote alipo na kufikishwa katika vyombo vya sheria. Baada ya kikao kumalizika baadhi ya wahusika kutoka kampuni iliyopewa kandarasi ya Kihanga Farm na wataalam wa maji wa serikali walioshiriki walikabidhiwa kwa vyombo husika ili kusaidia zaidi kwa taarifa muhimu.

Mhe. Aweso (Mb) amesema hakuna faida ya kuwa na mtalaam wa maji anayekabidhiwa mradi bila kujiridhisha na ubora wake kama taratibu zinavyotaka, ambapo imebainika moja ya udhaifu katika mradi wa maji Ukalawa-Kitole ni kwenda kinyume na mkataba, na kutozingatia ushauri wa Mhandisi Mshauri wa mradi na kubadili mfumo wa kusukuma maji kutoka wa kutumia jenereta, kwenda mfumo wa kutumia nishati ya jua (solar) wakati mazingira ya mradi sio rafiki kwa mfumo wa nishati ya jua.

Mhe. Aweso (Mb) ameagiza kutokana na udhaifu ulioonekana katika mradi huo ameagiza timu aliyoiunda akiwa mkoani Mbeya mwezi Oktoba 2018, ipite katika mradi wa maji Ukalawa na mradi wa Lugenge ambao madakio ya maji mawili yamekamilika lakini mradi bado hauridhishi na ukiwa katika asilimia 60 ya kazi pamoja na Mkandarasi kuongezewa muda.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Maji na Umwagiliaji 
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiongea na watalaam wa maji, pamoja na baadhi ya wahusika walioshiriki katika ujenzi wa mradi wa maji Ukalawa-Kitole katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka (kulia). 
1. Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwasikiliza baadhi ya wananchi watakaofaidika na mradi wa maji Lugenge mkoani Njombe. 
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb ) akipewa maelezo kuhusu kazi iliyoanza ya utandikaji wa mabomba kutoka katika dakio la maji kwenda katika tanki katika mradi wa maji Lugenge,pichani kati ni MKuu wa Mkoa wa Njombe Mh  Christopher Ole Sendeka 
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akipokea mrejesho wa wananchi kuhusu kero ya maji kando ya tanki la maji lililokamilika la mradi wa maji Lugenge. Mkandarasi kapewa mwezi mmoja kuhakikisha maji yanafika katika tanki hilo. 
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiangalia mitambo katika mradi wa maji Kibena. 


Hivyo makala WALIOZEMBEA KUSIMAMIA,KUJENGA MRADI WA MAJI UKALAWA-KITOLE, MKOANI NJOMBE WATAKIWA KUISAIDIA POLISI

yaani makala yote WALIOZEMBEA KUSIMAMIA,KUJENGA MRADI WA MAJI UKALAWA-KITOLE, MKOANI NJOMBE WATAKIWA KUISAIDIA POLISI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WALIOZEMBEA KUSIMAMIA,KUJENGA MRADI WA MAJI UKALAWA-KITOLE, MKOANI NJOMBE WATAKIWA KUISAIDIA POLISI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/waliozembea-kusimamiakujenga-mradi-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WALIOZEMBEA KUSIMAMIA,KUJENGA MRADI WA MAJI UKALAWA-KITOLE, MKOANI NJOMBE WATAKIWA KUISAIDIA POLISI"

Post a Comment