title : Wajumbe Baraza la Wawakilishi wapatiwa mafunzo ya uzazi wa mpango
kiungo : Wajumbe Baraza la Wawakilishi wapatiwa mafunzo ya uzazi wa mpango
Wajumbe Baraza la Wawakilishi wapatiwa mafunzo ya uzazi wa mpango
KATIBU Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar akizungumza na kuwakaribisha Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika Mafunzu ya siku mbili ya Uzazi wa Mpango yalioandaliwa na Wizara ya Afya kupitia Kitengo shirikishi cha Afya ya Mama na Mtoto na Shirika linaloshughulikia idadi ya Watu Duniani UNFPA katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni Zanzibar.
KIKUNDI cha maigizo kutoka Tumbatu (TUMBATU HEALTH ASSOCIACTION) kikitoa burdani ya igizo la uzazi wa mpango mbele ya wajumbe wa Baraza hilo pichani hawapo katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni Zanzibar.
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, wa pili kulia Naibu Spika Mgeni Hassan Juma,Mwenyekiti wa Baraza Mwanaasha Khamis Juma na Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman wakifuaatilia kwa Umakini igizo lililokua likioneshwa na kikundi cha maigizo kutoka Tumbatu .
MENEJA Kitengo cha Afya ya Mama na Mtoto Dkt. Ali Omar Ali akiwasilisha mada ya Afya ya Uzazi na Ujinsia na Mchango wake katika kuboresha Afya ya Mama na Mtoto kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika khafla iliofanyika katika Ukumbi mdogo wa Baraza hilko Chukwani Zanzibar.
SHEKHE Abdalla Talib Abdalla akiwasilisha mada Uislamu na Uzazi wa Mpango kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika khafla iliofanyika katika Ukumbi mdogo wa Baraza hilko Chukwani Zanzibar.
WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Maafisa kutoka Wizara ya Afya na Shirika linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani waliohudhuria katika Mafunzo hayo yaliofanyika katika Ukumbi mdogo wa Baraza hilko Chukwani Zanzibar.
WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Maafisa kutoka Wizara ya Afya na Shirika linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani waliohudhuria katika Mafunzo hayo yaliofanyika katika Ukumbi mdogo wa Baraza hilko Chukwani Zanzibar.
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid akifungua Mafunzu ya siku mbili ya Uzazi wa Mpango yalioandaliwa na Wizara ya Afya kupitia Kitengo shirikishi cha Afya ya Mama na Mtoto na kushirikiana na Shirika linaloshughulikia idadi ya Watu Duniani UNFPA katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni Zanzibar.
Hivyo makala Wajumbe Baraza la Wawakilishi wapatiwa mafunzo ya uzazi wa mpango
yaani makala yote Wajumbe Baraza la Wawakilishi wapatiwa mafunzo ya uzazi wa mpango Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wajumbe Baraza la Wawakilishi wapatiwa mafunzo ya uzazi wa mpango mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/wajumbe-baraza-la-wawakilishi-wapatiwa.html
0 Response to "Wajumbe Baraza la Wawakilishi wapatiwa mafunzo ya uzazi wa mpango"
Post a Comment