title : WAFANYABIASHARA SOKO LA SAMAKI FERI WATOA YA MOYONI KUHUSU MILIONI 20/= WALIZOPEWA NA RAIS
kiungo : WAFANYABIASHARA SOKO LA SAMAKI FERI WATOA YA MOYONI KUHUSU MILIONI 20/= WALIZOPEWA NA RAIS
WAFANYABIASHARA SOKO LA SAMAKI FERI WATOA YA MOYONI KUHUSU MILIONI 20/= WALIZOPEWA NA RAIS
Na Agness Francis,globu ya jamii
WAFANYABIASHARA wa Soko la Samaki Feri jijini Dar es Salaam wametoa ya moyoni kwa kumpongeza na kumshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa kutimiza ahadi yake kwa kukabidhi Sh.Milioni 20 kwa ajili ya soko hilo.
Shukrani hizo za wafanyabiashara hao zimetolewa na Diwani wa Kata ya Kivukoni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya soko hilo Henry Massaba.
Akifafanua zaidi kwa waandishi wa habari kuhusu fedha ambazo zimetolewa na Rais kwa ajili ya wafanyabiashara wa soko hilo ,Massaba amesema Rais Magufuli ametimiza ahadi aliyoiiahidi kwa wadau hao Desemba 9 mwaka 2015.
"Rais wetu mpendwa alipokuja kufanya usafi katika eneo hili la soko la zone 8 aliahidi kutoa fedha,na tayari ametimiza ahadi,lazima tumshukuru," amesema.Ameongeza kuwa "fedha hizo Sh. milioni 20 zilizokabidhiwa kwa wadau wa soko hili zitatumika katika ujenzi wa ofisi ya kikundi cha Umoja wa Wavuvi Tanzania.
Aidha Massaba amesama Mama Janeth Magufuli pia aliongezea kutoa mchango mkubwa kwa wakinamama wajasiriliamali wa sokoni hapo ambapo yeye amewakabidhi milioni 5."Fedha hizo zilizotolewa kwa kinamama hao wa soko hilo la feri zitawasaidia kukuza mitaji na vikundi vyao katika biashara zao,"amesema Massaba .
Kwa upande wa Naibu Katibu wa soko hilo Abeid Bura amewashukuru viongozi wa Serikali ya Awamu ya tano kwa kutembelea sokoni na kutambua changamoto na mambo yanayoendelea.
Baadhi ya WAFANYABIASHARA wa Soko la Samaki Feri jijini Dar es Salaam wakiendelea na shughuli zao.
Hivyo makala WAFANYABIASHARA SOKO LA SAMAKI FERI WATOA YA MOYONI KUHUSU MILIONI 20/= WALIZOPEWA NA RAIS
yaani makala yote WAFANYABIASHARA SOKO LA SAMAKI FERI WATOA YA MOYONI KUHUSU MILIONI 20/= WALIZOPEWA NA RAIS Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAFANYABIASHARA SOKO LA SAMAKI FERI WATOA YA MOYONI KUHUSU MILIONI 20/= WALIZOPEWA NA RAIS mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/wafanyabiashara-soko-la-samaki-feri.html
0 Response to "WAFANYABIASHARA SOKO LA SAMAKI FERI WATOA YA MOYONI KUHUSU MILIONI 20/= WALIZOPEWA NA RAIS"
Post a Comment