title : UNAHITAJI KUPIMIWA ARDHI ?, UTARATIBU NI HUU.
kiungo : UNAHITAJI KUPIMIWA ARDHI ?, UTARATIBU NI HUU.
UNAHITAJI KUPIMIWA ARDHI ?, UTARATIBU NI HUU.
Ardhi iwe kiwanja au nyumba thamani yake hupanda pale inapokuwa imepimwa. Kupima ardhi ni kurasimisha ardhi. Faida nyingi hupatikana baada ya ardhi kuwa imerasimishwa. Baadhi ya faida ni kuwa ardhi hupanda thamani yake, kuweza kupata mkopo kwa urahisi, ardhi kutumika kama dhamana mahakamani, lakini kubwa ni kuwa na amani na uhakika wa ardhi yako kuwa eneo ulilopo linaruhusiwa kisheria, sio eneo hatarishi, sio eneo la miradi ya serikali, sio hifadhi ya barabara au barabara nk. Unakuwa na amani kuwa uko sehemu sahihi na salama.
Kupima ardhi ni hatua inayopitiwa pale unapoelekea kupata hati. Kila ardhi yenye hati imepimwa lakini si kila ardhi iliyopimwa ina hati.
UTRATIBU WA KUPIMIWA ARDHI.
1.Kuandika barua ya maombi ni hatua ya kwanza ambapo utatakiwa kumwandikia mkurugenzi wa halmashauri ukiomba kupimiwa eneo lako. Hii ni barua ya kawaida ya kiofisi isipokuwa ieleze majina yako kwa ukamilifu na ichambue anuani ya eneo ambalo linalotakiwa kupimwa kwa ukamilifu.Mkurugenzi unayetakiwa kumwandikia ni yule wa halmashauri ambamo ardhi inayotakiwa kupimwa imo. Kwa mfano kama ardhi iko wilaya ya kinondoni basi mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya atakayeandikiwa barua.
Barua hiyo itaambatanishwa na nyaraka za umiliki wa eneo husika. Mara nyingi nyaraka hapa huwa ni ile mikataba ya mauziano. Kadhalika, barua yako inatakiwa kupitishwa serikali za mitaa na kwa mtendaji kata.
KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com
Hivyo makala UNAHITAJI KUPIMIWA ARDHI ?, UTARATIBU NI HUU.
yaani makala yote UNAHITAJI KUPIMIWA ARDHI ?, UTARATIBU NI HUU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UNAHITAJI KUPIMIWA ARDHI ?, UTARATIBU NI HUU. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/unahitaji-kupimiwa-ardhi-utaratibu-ni.html
0 Response to "UNAHITAJI KUPIMIWA ARDHI ?, UTARATIBU NI HUU."
Post a Comment