title : TANZANIA YAONGEZA TOZO BIDHAA YA MAZIWA.
kiungo : TANZANIA YAONGEZA TOZO BIDHAA YA MAZIWA.
TANZANIA YAONGEZA TOZO BIDHAA YA MAZIWA.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Serikali ya Tanzania imeongeza tozo ya kuingiza maziwa na bidhaa zake kwa zaidi ya asilimia 1,200, hatua ambayo imezua mjadala kuhusu hatima ya sekta ya maziwa nchini humo.
Hatua hiyo imezua mtafaruku kiasi cha wadau katika sekta hiyo kukutana kuijadili kuhusu hatua hiyo.
Tozo hiyo ambayo ipo katika kanuni zilizotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilipitishwa mwezi Agosti, lakini ikaanza kutekelezwa Oktoba I mwaka huu.
Awali, waagizaji walikuwa wanalipa Sh150 kwa kilo moja ya maziwa iliyoingizwa Tanzania, lakini sasa ada hiyo imepanda hadi Sh2,000, ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 1,233.
Baadhi wanahisi wamebainisha kuwa hatua hiyo inalenga kuzuia maziwa yanayoagizwa kutoka nje, hasa Kenya pamoja na Afrika Kusini.
"Hizi si kanuni bali ni marufuku ya kuingiza maziwa nchini. Haiwezekani tozo ikapanda kwa kiasi hicho, bidhaa zetu hazitauzika tena," amesema Mkurugenzi wa kampuni ya Woodland Dairy nchini Kariras Alando.
Kampuni hiyo ina makao makuu yake yapo nchini Afrika Kusini na huuza maziwa aina ya First Choice.
Hata hivyo serikali ya Tanzania imesema ongezeko la tozo hiyo ni la kawaida na wala halina lengo la kumuonea mtu.
Mchambuzi wa masuala ya kiuchumi, Lenny Kasoga, amesema iwapo hatua hizo zimechukuliwa kuimarisha soko la ndani ndani ambapo maziwa yalikuwa yanatoka hazitachukua hatua za kulipiza kisasi kama inavyofanyika kwa Marekani na Uchina, basi itakuwa na manufaa.
"Wazalishaji watazalisha kwa wingi zaidi na maziwa yakauzwa. Watanufaika na soko la ndani bila ushindani wa nje. Lakini kwa upande mwingine ushindani hufaa, unapopata mshindani unaweza ukajitahidi kuboresha zaidi ubora wa bidhaa zako, kusudi upate hata soko la nje," amesema.
Kasoga amesema kuwa wasiwasi pia kwamba huenda taifa likawa halijajiandaa vya kutosha kukidhi mahitaji ya soko la maziwa.
"Huko vijijini hali bado ni duni, wale walio na ng'ombe ndio wanaotumia maziwa...sasa hivi kauli mbiu ni viwanda na kuongeza pato tufike katika pato la kati. Je, mmejipanga? Unapokurupuka na haujajipanga, matokeo yako ni kwamba wanaoumia ni wananchi."
"Kuna wanaosema tumekomaa kiasi kwamba tujitegemee kwa kuzalisha ndani na kutozana kodi gani, mwananchi wa kawaida huwa hajali. Unapokuja wa wachumi ndipo kunatokea maswali, maamuzi yaliyochukuliwa yamemlenga nani, yatamfadi nani na kwa kipindi gani?"
Shirika la Afya Duniani (WHO) likipendekeza unywaji wa walau lita 200 kwa mwaka, takwimu zinaonyesha kuwa kila Mtanzania hunywa wastani wa lita 45 tofauti na Wakenya wanaokunywa lita 145.
Kwa hatua hiyo, wateja waliokuwa wananunua kopo la lita moja kwa Sh3,200 sasa hivi bei itapanda kwa zaidi ya asilimia 75 hivyo kutakiwa kulipa takriban Sh6,000 kwa kiasi hicho hicho.
Unywaji wa maziwa Tanzania
Kiwango cha unywaji wa maziwa Tanzania bado kiko chini ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki.
Shirika la Chakula Duniani (FAO) linapendekeza lita 200 zinywewe kwa mtu mmoja kwa mwaka lakini nchini Tanzania kiwango hicho kwa sasa ni wastani wa lita 6 hadi 45 kwa mtu mmoja kwa mwaka.
Nchini Kenya, kiwango hicho ni kati ya lita 19 maeneo ya mashambani hadi lita 125 maeneo ya mijini.
Takwimu za Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) zinaonyesha Kenya ina ng'ombe wa maziwa 5 milioni ikiizidi Tanzania kwa zaidi ya ng'ombe 4 milioni.
Hata hivyo Tanzania ni nchi yenye nafasi nzuri ya kuzalisha maziwa kwa wingi, lakini bado haijaweza kutumia nafasi hiyo kikamilifu.
Kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia ya mwaka 2008 iliyolinganisha sekta ya maziwa India, Uganda na Tanzania.
Wakati Uganda inakisiwa kujitosheleza kwa maziwa, kiasi kikubwa cha maziwa yaliyo katika soko rasmi nchini Tanzania huagizwa kutoka nje.
Nchini Tanzania, ingawa uzalishaji wa maziwa unaongezeka, na sekta isiyo rasmi ni kubwa zaidi, lakini baadhi ya changamoto zilizopo ni kushindwa kwa sekta kukabiliana na tatizo la kuyumba kwa kiwango cha uzalishaji kutoka msimu mmoja hadi mwingine, uhaba wa takwimu ambazo ni muhimu katika kuweka mipango na kuendesha sehemu mbalimbali za mtiririko wa thamani.
Kadhalika, kuna tatizo la uwezo mdogo na uchache wa vikundi vya wafugaji, wasindikaji, wafanya biashara viwe vya ushirika au umoja, na mtandao mbovu wa barabara vijijini.
Maziwa huzalishwa kwa wingi wakati wa masika, lakini kiasi kikubwa (asilimia 20 hadi 50) huharibika kutokana na kukosa soko. Wakati wa kiangazi kiwango cha uzalishaji hushuka na kushindwa kukidhi mahitaji ya soko.
Ukuaji wa sekta ya maziwa Tanzania pia unakwamishwa na wingi wa sheria na kanuni ambazo huongeza gharama za kuendesha biashara na pia mfumo wa kodi ambao unamwongezea mlaji mzigo wa bei ya bidhaa za maziwa yaliyosindikwa na sekta rasmi.
Hivyo makala TANZANIA YAONGEZA TOZO BIDHAA YA MAZIWA.
yaani makala yote TANZANIA YAONGEZA TOZO BIDHAA YA MAZIWA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANZANIA YAONGEZA TOZO BIDHAA YA MAZIWA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/tanzania-yaongeza-tozo-bidhaa-ya-maziwa.html
0 Response to "TANZANIA YAONGEZA TOZO BIDHAA YA MAZIWA."
Post a Comment