TAASISI YA HASSAN MAAJAR YAKABIDHI VYOO SHULE YA MSINGI PUGU KAJIUNGENI

TAASISI YA HASSAN MAAJAR YAKABIDHI VYOO SHULE YA MSINGI PUGU KAJIUNGENI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TAASISI YA HASSAN MAAJAR YAKABIDHI VYOO SHULE YA MSINGI PUGU KAJIUNGENI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TAASISI YA HASSAN MAAJAR YAKABIDHI VYOO SHULE YA MSINGI PUGU KAJIUNGENI
kiungo : TAASISI YA HASSAN MAAJAR YAKABIDHI VYOO SHULE YA MSINGI PUGU KAJIUNGENI

soma pia


TAASISI YA HASSAN MAAJAR YAKABIDHI VYOO SHULE YA MSINGI PUGU KAJIUNGENI

Taasisi ya Hassan Maajar Trust (HMT), imeendeleza dhamira yake ya kuboresha mazingira ya shule za msingi nchini, ambapo imekabidhi jengo la vyoo shule ya msingi Pugu Kajiungeni, wilaya ya Ilala, Dar es Salaam. Jengo hilo lililogharimu jumla ya Shillingi milioni 65,000.00 lina vyumba 12 na sehemu maalumu kwa wavulana -urinals, ambapo vyumba 2 ni kwa ajili ya ya watoto wenye ulemavu na chumba cha staha kimoja (Dignity Room) kwa ajili ya wasichana wenye mahitaji ya staha. 
 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar, Balozi Mwanaidi Maajar, alikabidhi vyoo hivyo kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bi. Rophina Aloyce Kawishe, katika hafla fupi iliyohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema, ambaye alikuwa mgeni rasmi, walimu, wanafunzi, na wawakilishi kutoka Shirika la Water Aid. 
 
Akiongea katika hafla hiyo, Balozi Maajar amesema “Hii ni mara ya kwanza kwa HMT kujenga vyoo vya shule, na tumefurahia kukamilisha mradi huu wa kwanza. Kwa kipindi kirefu nyuma, HMT ilikuwa inajulikana kwa kampeni yake kubwa ya ‘Dawati Kwa Kila Mtoto’ ambayo imefanikiwa kwa kutoa madawati 10,000, na kunufaisha zaidi ya wanafunzi 30,000 katika mikoa 13 nchini. 
 
Tuliona vilevile vile kuna changamoto ya uhaba wa vyoo mashuleni. Imekuwa fursa nyingine ya Taasisi ya HMT na wafadhili wake kuunga nguvu kwa pamoja kwa kampeni mpya yenye kauli mbiu, Vyoo Bora Kila Shule. Aidha amesema, kila safari ni hatua ya kwanza na kwa mradi huu ndiyo hatua ya kwanza kwa HMT kutimiza lengo la kujenga vyoo shule za msingi zilizo na mahitaji na hasa shule zilizo na idadi kubwa ya wanafunzi wenye ulemavu.  

Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar, Balozi Mwanaidi Maajar akitoa hotuba wakati wa hafla ya uzunduzi wa miundo mbinu ya vyoo katika shule ya msingi ya Pugu Kajiungeni ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya  ya Ilala,Sophia mjema, Hafla hiyo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu, walimu, wanafunzi, Maofisa ma maofisa kutoka taasisi ya HMT 

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema( katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la Vyoo bora 12 na vyumba Viwili kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Pugu Kajiungeni jijini Dar es Salaa, Wengine kwenye picha ni mwenyekiti wa Hassan Maajar Trust (TMT) Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (wapili kulia) Mkuu wa shule ya msingi Pugu Kajiungeni,Ropiana Alponce (Kushoto) pamoja na viongozi wengine, Msaada huo umejengwa na Taasisi ya Hassan Maajar Trust. 

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akihutubia wageni waalika katika hafla hiyo. 

Wanafunzi wasichana wakipokea baadhi ya zawadi zilizotolewa na marafiki wa taasisi ya HMT wakati wa hafla hiyo. 

Mgeni rasmi akikagua miundombinu ya choo cha kisasa kilichojengwa na HMT chini ya mpango wake wa Vyoo Bora kwa Kila shule.



Hivyo makala TAASISI YA HASSAN MAAJAR YAKABIDHI VYOO SHULE YA MSINGI PUGU KAJIUNGENI

yaani makala yote TAASISI YA HASSAN MAAJAR YAKABIDHI VYOO SHULE YA MSINGI PUGU KAJIUNGENI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TAASISI YA HASSAN MAAJAR YAKABIDHI VYOO SHULE YA MSINGI PUGU KAJIUNGENI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/taasisi-ya-hassan-maajar-yakabidhi-vyoo.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TAASISI YA HASSAN MAAJAR YAKABIDHI VYOO SHULE YA MSINGI PUGU KAJIUNGENI"

Post a Comment