title : NEWS ALERT: HANS POPPE APANDISHWA KIZIMBANI LEO, AACHIWA KWA DHAMANA
kiungo : NEWS ALERT: HANS POPPE APANDISHWA KIZIMBANI LEO, AACHIWA KWA DHAMANA
NEWS ALERT: HANS POPPE APANDISHWA KIZIMBANI LEO, AACHIWA KWA DHAMANA
Na Ripota Maalum, blogu ya jamii.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba, Zacharia Hanspope, amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka mawili kabla ya kuachiwa kwa dhamana.
Hanspope leo Oktoba 16, 2018 ameunganishwa katika kesi ya kughushi nyaraka za klabu na utakatishaji wa fedha inayomkabili Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu
Baada ya kuunganishwa katika kesi hiyo, Wakili wa Serikali, Shadrack Kimaro amewasomea washtakiwa wote, mashtaka 10 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba. Katika mashitaka hayo 10, Hanspope anakabiliwa na mashtaka 2, shtaka moja ni la kuwasilisha nyaraka za uongo na shtaka jingine ni kughushi.
Katika mashtaka hayo 10, yamo ya kula njama, kutoa nyaraka za uongo, matumizi mabaya ya madaraka, kughushi, utakatishaji, kuwasilisha nyaraka za kughushi na kuendesha biashara bila kufuata sheria. Katika shitaka la utakatishaji Aveva na Kaburu wanahusishwa na shtaka la kutakatisha kiasi cha dola 300,000 (zaidi ya sh. Milioni 650)
Katika shitaka la kughushi linawakabili washtakiwa wote, imedaiwa Machi 15, 2016 washtakiwa kwa pamoja walighushi hati ya malipo ya kibiashara ya Mei 28, 2016 wakionyesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zinathamani ya dola 40,577, zaidi ya Sh. Milioni 90 huku wakijua kwamba sio kweli.
Pia katika shtaka jingine inadaiwa Aveva, Nyange na Hans Poppe kati ya March10 na Septemba 30, 2016 waliwasilisha nyaraka za uongo kuonyesha Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Kimarekani 40,577.
Hata hivyo, shtaka la mwisho halikusomwa kwa sababu linamuhusu mshtakiwa 4 Lauwo ambaye bado hajafikishwa mahakamani.
Baada ya kusomewa mashtaka yao Mahakama ilitoa masharti ya dhamana kwa Hanspope yaliyomtaka kuwa na wadhamini wawili watakaosaini Bondi ya Sh.milioni 15 kila mmoja,
Mshtakiwa alifanikiwa kutimiza masharti ya dhamana na kuachiwa huku Aveva na Kaburu wakirudishwa rumande kwa kuwa mashtaka dhidi yao hayana dhamana.
Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 10.
Hivyo makala NEWS ALERT: HANS POPPE APANDISHWA KIZIMBANI LEO, AACHIWA KWA DHAMANA
yaani makala yote NEWS ALERT: HANS POPPE APANDISHWA KIZIMBANI LEO, AACHIWA KWA DHAMANA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NEWS ALERT: HANS POPPE APANDISHWA KIZIMBANI LEO, AACHIWA KWA DHAMANA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/news-alert-hans-poppe-apandishwa.html
0 Response to "NEWS ALERT: HANS POPPE APANDISHWA KIZIMBANI LEO, AACHIWA KWA DHAMANA"
Post a Comment