title : NAIBU WAZIRI WA NISHATI AKABIDHI SOLAR POWER KWA ZAHANATI TATU ZA HALMASHAURI YA CHALINZE
kiungo : NAIBU WAZIRI WA NISHATI AKABIDHI SOLAR POWER KWA ZAHANATI TATU ZA HALMASHAURI YA CHALINZE
NAIBU WAZIRI WA NISHATI AKABIDHI SOLAR POWER KWA ZAHANATI TATU ZA HALMASHAURI YA CHALINZE
Na Victor Masangu, Chalinze
WANAWAKE wa kijiji cha Mduma kata Magindu katika halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani kwa sasa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kutokuwa na nishati ya umeme hivyo inawalazimu kupatiwa matibabu kwa kutumia mwanga wa tochi au simu pindi wanapokwenda kujifungua katika zahanati ya Mduma kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa maisha yao.
Wakizungumza kijijini hapo kuhusiana na changamoto inayowakabili wanawake hao wamesema kwamba kwa sasa wanapata shida kubwa wakati wa kujifungua hasa katika nyakati za usiku kutokana na kuwa na giza hivyo kuwapa wakati mgumu wauguzi pindi wanapotekeleza majukumu yao.
Aidha walisema kwamba kwa kipindi kirefu katika zahanati hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbali mbali za upatikanaji wa utoaji wa huduma kwa wagonjwa hivyo wameiomba serikali ya awamu ya tano kuingilia kati suala hilo kwa lengo la kuweza kuwafikishia nishati ya umeme ambayo itakuwa ni mkombozi katika utoaji wa huduma hasa katika nyakati za usiku.
Kwa upande wake mmoja wa wauguzi katika zahanati ya Mduma Neema Muhagama amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ya kutokuwa na nishati ya umeme hivyo inawapelekea wakati mwingine kutumia mwanga wa tochi za simu katika kuwapatia matibabu wagonjwa hasa kwa upande wa wakinamama wajawazito pindi wanapohitaji kujifungua.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu wa katikati ambaye pia ni Mbunge wa viti maalumu (CCM) kutoka Mkoa wa Pwani akikabidhi msaada wa Solar Power kwa baadhi ya wauguzi wa zahanati ya Mduma iliyopo kata ya Kibindu katika halmashauri ya Chalinze iliyopo Wilayani Bagamoyo kulia kwake ni muuguzi Neema Muhagama akipokea kwa niaba ya wenzake.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Naibu Waziri wa nishati Subila Mgalu wa kulia ambaye pia ni Mbunge wa viti maalumu (CCM) kutoka Mkoa wa Pwani akimkabidhi msaada wa Solar Power Martha Kilimba ambaye ni mmoja wa wauguzi katika zahanati ya Kwamsanja iliyopo kata ya Kibindu katika halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo kwa lengo la kuwasaidia wagonjwa ambao wamekuwa wakipata adha ya kutibiwa kwa kutumia mwanga wa tochi za simu.
Naibu waziri wa nishati Subira Mgalu kulia ambaye pia ni Mbunge wa viti maalumu (CCM) kutoka Mkoani Pwani akimkabidhi msaada wa Solar Power mmoja wa wauguzi katika zahanati ya Kibindu iliyopo kata ya Kibindu katika halmashauri ya Chalinze iliyopo Wilayani Bagamoyo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala NAIBU WAZIRI WA NISHATI AKABIDHI SOLAR POWER KWA ZAHANATI TATU ZA HALMASHAURI YA CHALINZE
yaani makala yote NAIBU WAZIRI WA NISHATI AKABIDHI SOLAR POWER KWA ZAHANATI TATU ZA HALMASHAURI YA CHALINZE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI WA NISHATI AKABIDHI SOLAR POWER KWA ZAHANATI TATU ZA HALMASHAURI YA CHALINZE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/naibu-waziri-wa-nishati-akabidhi-solar.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI WA NISHATI AKABIDHI SOLAR POWER KWA ZAHANATI TATU ZA HALMASHAURI YA CHALINZE"
Post a Comment