title : NAIBU WAZIRI NDITIYE ATEMBELEA MRADI WA DGMP BANDARINI
kiungo : NAIBU WAZIRI NDITIYE ATEMBELEA MRADI WA DGMP BANDARINI
NAIBU WAZIRI NDITIYE ATEMBELEA MRADI WA DGMP BANDARINI
Na Leonard Magomba
MRADI mkubwa wa kuboresha Bandari ya Dar es Salaam ‘Dar es Salaam Maritime Gateway Program’ (DGMP) umefikia asimilia 42 ya ujenzi wake hadi sasa.
Mradi huo unahusisha ujenzi wa gati maalum ya kushushia magari (RORO), gati Na. 1-7, kuongeza kina cha maji katika magati hayo pamoja na kutanua lango la kuingia meli bandarini.
Mradi huo ambao umelenga kuifanya Bandari ya Dar es Saalam kuwa ya kisasa zaidi na kuongeza uwezo wake wa kuhudumia meli kubwa kwa wakati mmoja unatarajia kukamilika mwezi Juni, 2020.
Hayo yamebainika leo wakati Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye alipotembelea mradi huo bandarini ili kukagua maendeleo ya ujenzi wake.
“Nimefurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa mradi huu ambao hadi sasa umefikia asilimia 42 amesema Mh. Nditiye na kuongeza kwamba matarajio yetu mradi huu utaisha kwa wakati uliopangwa.”
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Karim Mattaka akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye kuhusu ujenzi wa maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam alipofika eneo la kutengenezea zege linalotumika kwa ajili ya ujenzi huo.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Karim Mattaka akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa gati namba moja (1) ya Bandari ya Dar es Salaam kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye mara baada ya Waziri huyo kufanya ziara bandarini kukagua mradi huo.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Karim Mattaka akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye mara baada ya kufika katika moja ya maabara zinazotumika kupima udongo kwa ajili ya ujenzi huo bandarini.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
Hivyo makala NAIBU WAZIRI NDITIYE ATEMBELEA MRADI WA DGMP BANDARINI
yaani makala yote NAIBU WAZIRI NDITIYE ATEMBELEA MRADI WA DGMP BANDARINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI NDITIYE ATEMBELEA MRADI WA DGMP BANDARINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/naibu-waziri-nditiye-atembelea-mradi-wa.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI NDITIYE ATEMBELEA MRADI WA DGMP BANDARINI"
Post a Comment