title : NAIBU WAZIRI MABULA AMKABIDHI BIBI MASINGE HATI ZA VIWANJA VIWILI
kiungo : NAIBU WAZIRI MABULA AMKABIDHI BIBI MASINGE HATI ZA VIWANJA VIWILI
NAIBU WAZIRI MABULA AMKABIDHI BIBI MASINGE HATI ZA VIWANJA VIWILI
Na Munir Shemweta, Mara
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula amemkabidhi Bibi Nyasasi Masige Hati za viwanja viwili vilivyopo eneo la Bunda mkoa wa Mara na kutoa onyo kwa wataalamu wa ardhi kutotoa ushauri potofu kwa viongozi wa serikali wakati wa utekelezaji wa majukumu ya sekta ya ardhi.
Utoaji wa hati kwa bibi Masige unafuatia bibi huyo kuwasilisha malalamiko kwa mhe Rais John Pombe Magufuli wakati wa ziara yake katika wilaya ya Bunda mkoa wa Mara kutaka kudhulumiwa viwanja vyake. Hati za viwanja alivyokabidhiwa bibi Masige ni za viwanja Na 92 na 93/ Kitalu S/ Nyasula C vilivyopo katika wilaya ya Bunda mkoa wa Mara.
Mabula alikabidhi hati hizo pamoja na hati nyingine 92 kwa wananchi wa Bunda leo akiwa katika ziara ya siku tano katika mkoa wa Mara kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyatoa katika ziara yake ya februari mwaka huu 2018 katika mkoa wa Mara.
Alisema serikali inategemea wataalamu katika kuendesha shughuli zake na kitendo cha wataalamu kutoa ushauri potofu ikiwemo suala la viwanja vya bibi Masige siyo tu kunawapoteza viongozi katika kutekeleza majukumu yao bali kunachangia kuwepo migogoro katika sekta ya ardhi.
"haiwezekani kupima viwanja na kuchanganya viwanja vidogo, vikubwa na vya kati na kama mtaalamu ukienda kinyume utachukuliwa hatua kwa kutozingatia taaluma."" Alisema Mabula.
Kauli hiyo ya Mabula inafuatia Kauli ya Mkuu wa wilaya ya Bunda Lydia Mpilipili kueleza kuwa tatizo la viwanja vya bibi Masige lisingefikia hatua hiyo kama wataalam wa ardhi wangetoa ushauri sahihi kwa viongozi wa wilaya katika kushugulikia mgogoro wa bibi huyo.
Bibi Nyasasi Masige akipelekwa na ndugu zake kwa ajili ya kukabidhiwa hati za viwanja vyake na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Angeline Mabula leo wilayani Bunda mkoani Mara.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula akimpa mkono Bibi Nyasasi Masige mara baada ya kumkabidhi hati za viwanja vyake wilayani Bunda mkoa wa Mara leo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la rais kushughulikia tatizo la bibi huyo.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula akimkabidhi hati ya kiwanja mmoja wa wakazi wa Wilaya ya Bunda mkoa wa Mara Joseph Matundilo wakati wa ziara yake ya siku tano mkoani humo kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa wakati wa ziara yake ya Februari 2018.
Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula akizungumza na viongozi na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri mbili za wilaya ya Bunda mkoani Mara wakati wa ziara yake ya siku tano kufuatilia utekelezaji wa maagizo yake aliyoyatoa wakati wa ziara ya Februari 2018. (Picha zote na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala NAIBU WAZIRI MABULA AMKABIDHI BIBI MASINGE HATI ZA VIWANJA VIWILI
yaani makala yote NAIBU WAZIRI MABULA AMKABIDHI BIBI MASINGE HATI ZA VIWANJA VIWILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI MABULA AMKABIDHI BIBI MASINGE HATI ZA VIWANJA VIWILI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/naibu-waziri-mabula-amkabidhi-bibi.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI MABULA AMKABIDHI BIBI MASINGE HATI ZA VIWANJA VIWILI"
Post a Comment