NAIBU WAZIRI HASUNGA AONYA UKATAJI MITI HOVYO MKOANI SONGWE

NAIBU WAZIRI HASUNGA AONYA UKATAJI MITI HOVYO MKOANI SONGWE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NAIBU WAZIRI HASUNGA AONYA UKATAJI MITI HOVYO MKOANI SONGWE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NAIBU WAZIRI HASUNGA AONYA UKATAJI MITI HOVYO MKOANI SONGWE
kiungo : NAIBU WAZIRI HASUNGA AONYA UKATAJI MITI HOVYO MKOANI SONGWE

soma pia


NAIBU WAZIRI HASUNGA AONYA UKATAJI MITI HOVYO MKOANI SONGWE



Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga amewaonya watu wenye tabia ya kukata miti ovyo kuwa Serikali hatosita kuwachukulia hatua za kisheria kutokana na kushamiri kwa uharibifu wa misitu mkoani Songwe.

Ametoa onyo hilo wakati alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Isalalo kata ya Wasa wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe. Amesema kufuatia kasi ya ukataji miti ovyo unaoendelea kwa ajili ya mbao na nishati ya mkaa katika maeneo hayo kunatishia kutoweka kwa mvua wanayoitegemea kwa ajili kilimo cha mazao ya kahawa, mahindi pamoja na mazao mengine.

Amewaeleza Wananchi hao kuwa uharibifu huo ukiendelea utaawathiri wao wenyewe kwa vile mvua itakoma kunyesha katika maeneo yao. Amewataka wakikata mti wapande miti na wale wanaokata miti kwa ajili ya Nishati ya mkaa wafuate kanuni na sheria ili kuepuka kukabiliana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)

Aidha, Mhe. Hasunga Amewataka Wananchi hao kuwa hata pale inapotokea wanataka kukata mti wa mwembe uliopo katika nyumba zao wanatakiwa kuomba kibali kutoka TFS. Pia, Waziri Hasunga amewaagiza TFS itoe miche 10,000 kwa Kata ya Wasa msimu wa mvua utakapokaribia kufuatia ombi la mwanakijji Kasian Mwanjala alilowasilisha kwa Mhe. Hasunga kuwa wanataka kupanda miti ili wanakosa miche.

Katika hatua nyingine, Mhe.Hasunga ambaye ni Mbunge katika jimbo la Vwawa lililopo mkoani hapo amewahakikishia wananchi wake kuwa ifikapo mwakani kata ya Wasa itapata umeme wa REA hali itakayosaidia kuboresha maisha kwa wananchi wake. “Moja ya ahadi yangu niliyoitoa kwenu ni kuhakikisha katika jimbo langu wananchi mnapata umeme, hadi sasa tayari nguzo za umeme zimeanza kuwekwa ” amesema Mhe Hasunga.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza jana na wananchi kuhusu athari za ukataji miti ovyo kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Isalalo kata ya Wasa wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe. 
Baadhi ya Watendaji aliokuwa ameongozana nao katika mkutano huo wa hadhara katika kijiji cha Isalalo. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akimsikiliza huku akiwa anaandika swali analoulizwa na zungumza Ester Mwakanja kuhusiana athari za ukataji miti ovyo kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Isalalo kata ya Wasa wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akisoma karatasi katika mkutano wa hadhara ulioufanya katika kijiji cha Isalalo kata ya Wasa wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe .( PICNA NA LUSUNGU HELELA) 


Hivyo makala NAIBU WAZIRI HASUNGA AONYA UKATAJI MITI HOVYO MKOANI SONGWE

yaani makala yote NAIBU WAZIRI HASUNGA AONYA UKATAJI MITI HOVYO MKOANI SONGWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI HASUNGA AONYA UKATAJI MITI HOVYO MKOANI SONGWE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/naibu-waziri-hasunga-aonya-ukataji-miti.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NAIBU WAZIRI HASUNGA AONYA UKATAJI MITI HOVYO MKOANI SONGWE"

Post a Comment