title : Naibu Meya Ilala atoa tani moja ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi
kiungo : Naibu Meya Ilala atoa tani moja ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi
Naibu Meya Ilala atoa tani moja ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akiwa na mwenyeji wake Diwani wa kata ya Mzinga JOB IZAC wakati wa kukagua kituo cha Polisi kilichojengwa kwa nguvu ya wananchi Kata ya Mzinga Wilayani Ilala ambapo Naibu Meya Kumbilamoto katika ziara yake alikabidhi tani moja ya Seruji kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa kituo hicho kinachotarajia kukamilika Desemba mwaka huu.Picha na Heri shaaban.
Mwambawahabari
Na Heri Shaaban
NAIBU Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto ametoa tani moja ya cement,kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi cha Kisasa Kata ya Mzinga Wilayani Ilala.
Akikabidhi tani moja ya seruji Naibu Meya Kumbilamoto aliwataka wadau wa Manispaa ya Ilala na wengine wapenda maendeleo kuunga mkono juhudi za Serikali katika suala la ulinzi na usalama .
"Suala la Ulinzi na usalama letu sote wananchi wanaitaji usalama nampongeza Mkuu wa wilaya ya Ilala
Sophia Mjema pamoja na Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Paul Makonda kusogeza huduma karibu na wananchi kituo hichi kikifunguliwa wananchi watahudumiwa eneo lao "alisema Kumbilamoto.
Amewapongeza wakazi wa Mzinga na Uongozi wa kata hiyo pamoja na Mwanagati yetu kwa kufanikisha ujenzi huo.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi Godfrey Mjungu alisema kituo hicho cha kisasa kitagharimu shilingi milioni 250 ni pesa za wananchi mchakato wake ulianza wakati wa Kamanda Seleman Kova ..
Naye Diwani wa kata ya Mzinga Job Issack alisema kituo hicho kikikamilika kitakuwa kinahudumia wakazi wa Mzinga,Chanika,Msongola na wakazi wa mpaka wa Temeke na Ilala kwani kinauwezo mkubwa na kitakuwa kinapokea mahabusu wengi
Diwani Job Issack alisema katika kata hiyo,kuna wakazi 32000 kwa mujibu wa Sensa iliyopita ya makazi.
Alisema ujenzi wa kituo hicho ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya chama kwa ajili ya kuwasogezea huduma wananchi wa Mzinga.
Hivyo makala Naibu Meya Ilala atoa tani moja ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi
yaani makala yote Naibu Meya Ilala atoa tani moja ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Naibu Meya Ilala atoa tani moja ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/naibu-meya-ilala-atoa-tani-moja-ya.html
0 Response to "Naibu Meya Ilala atoa tani moja ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi"
Post a Comment