title : MWENYEKITI WA KAMATI YA UONGOZI WA TASAF UNGUJA AMBAE PIA NI MKUU WA MKOA WA MJINI MAGHARIB ATEMBELEA KITUO KIPYA CHA AFYA KIANGA WILAYA YA MAGAHARIBA ‘A’.
kiungo : MWENYEKITI WA KAMATI YA UONGOZI WA TASAF UNGUJA AMBAE PIA NI MKUU WA MKOA WA MJINI MAGHARIB ATEMBELEA KITUO KIPYA CHA AFYA KIANGA WILAYA YA MAGAHARIBA ‘A’.
MWENYEKITI WA KAMATI YA UONGOZI WA TASAF UNGUJA AMBAE PIA NI MKUU WA MKOA WA MJINI MAGHARIB ATEMBELEA KITUO KIPYA CHA AFYA KIANGA WILAYA YA MAGAHARIBA ‘A’.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa TASAF Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib akipatiwa maelezo na Mkurugenzi Uratibu shughuli za Serikali Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Khalid Bakar (alievaa suti nyeusi) alipofanya ziara ya kutembelea kituo cha afya Kianga Wilaya ya Magharib ‘A’ Unguja.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya TASAF Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib akizungumza na Wananchi wa Kianga (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kutembelea kituo cha Afya cha Kijiji hicho.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kianga wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya TASAF Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib baada ya kutembelea ujenzi wa kituo chao kipya cha afya.
Muonekano wa Kituo kipya cha Afya cha kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharib ‘A’ Unguja ambacho kiko katika hatua za mwisho kumalizika.Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.
Na Mwashungi Tahir - Maelezo. 12-10-2018.
Mwenyekiti wa kamati ya Uongozi wa TASSAF Unguja
Ayoub Mohamed Mahmoud amesema kumalizika kwa kituo
cha afya Shehia ya Kianga Wilaya ya Magharib “B” kitatoa
huduma kwa wananchi wa maeneo ya shehia hiyo na
majirani.
Akizungumza na wananchi wa shehia ya Kianga alipokuwa
akikagua kituo cha afya cha shehia hiyo na kuona jinsi
kinavyoendelea na ujenzi wa mradi huo amesema ni juhudi
za wananchi wa shehia ya Kianga wilaya ya Magharib A .
Alisema kituo hicho kitakapomalizika tayari watumishi
wanaostahiki wataletwa wa kutosha kwa kutoa huduma kwa
wananchi wa Shehia hiyo kwa ajili ya kupata matibabu kwa
lengo la kuondoshewa usumbufu .
“Kituo kitakapomalizika msiwe na wasiwasi tayari
wafanyakazi watakuwepo kwa kufanya kazi hiyo na ufanisi
zaidi ili kuona wananchi wanapata huduma hiyo kwa
urahisi”.Alisema Mwenyekiti huyo ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Mkoa wa Mjini Magharib.
Pia alisema mashirikiano ya Serikali zote mbili ikiwemo ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa inaboresha Vituo vya Afya
kwa kuwasogezea karibu na wanamoishi ili wananchi
waweze kufaidika na huduma hiyo mjini na vijijini bila ya
usumbufu.
Nae sheha wa Shehia ya Kianga Juma Issa Juma alisema
wanashukuru kupata mradi wa TASSAF kwa kuwapatia
kituo hicho cha Afya ambacho kitakapomalizika tutafaidika
kwa kupata huduma hii kwa urahisi zaidi.
Alisema wananchi wa Kianga watafaidika kwa asilimia mia
moja kwani ugonjwa hauna muda maalum lakini kituo kipo
hapa madaktari watakuwepo tutakuwa wenye kufaidika na
matunda ya nchi yetu kwa kupitia viongozi wetu wa nchi.
Vile vile sambamba na hayo mwananchi wa shehia hiyo
Subira Mohamed Jecha amesema kwa sasa tumo furahani
wananchi sote hasa akinamama kwani kutatupunguzia
masafa marefu ya kufatia huduma hiyo ya Afya tukiwa na
watoto au wajawazito kwani huduma hii tunaifata Mwera au
Kizimbani.
Mwisho.
Imetolewa na idara ya Habari Maelezo.
Hivyo makala MWENYEKITI WA KAMATI YA UONGOZI WA TASAF UNGUJA AMBAE PIA NI MKUU WA MKOA WA MJINI MAGHARIB ATEMBELEA KITUO KIPYA CHA AFYA KIANGA WILAYA YA MAGAHARIBA ‘A’.
yaani makala yote MWENYEKITI WA KAMATI YA UONGOZI WA TASAF UNGUJA AMBAE PIA NI MKUU WA MKOA WA MJINI MAGHARIB ATEMBELEA KITUO KIPYA CHA AFYA KIANGA WILAYA YA MAGAHARIBA ‘A’. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MWENYEKITI WA KAMATI YA UONGOZI WA TASAF UNGUJA AMBAE PIA NI MKUU WA MKOA WA MJINI MAGHARIB ATEMBELEA KITUO KIPYA CHA AFYA KIANGA WILAYA YA MAGAHARIBA ‘A’. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/mwenyekiti-wa-kamati-ya-uongozi-wa.html
0 Response to "MWENYEKITI WA KAMATI YA UONGOZI WA TASAF UNGUJA AMBAE PIA NI MKUU WA MKOA WA MJINI MAGHARIB ATEMBELEA KITUO KIPYA CHA AFYA KIANGA WILAYA YA MAGAHARIBA ‘A’."
Post a Comment