MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU AWEKA WAZI NAMNA ATAKAVYOIENDESHA TAASISI HIYO NYETI YA KUPAMBANA NA WALA RUSHWA NCHINI

MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU AWEKA WAZI NAMNA ATAKAVYOIENDESHA TAASISI HIYO NYETI YA KUPAMBANA NA WALA RUSHWA NCHINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU AWEKA WAZI NAMNA ATAKAVYOIENDESHA TAASISI HIYO NYETI YA KUPAMBANA NA WALA RUSHWA NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU AWEKA WAZI NAMNA ATAKAVYOIENDESHA TAASISI HIYO NYETI YA KUPAMBANA NA WALA RUSHWA NCHINI
kiungo : MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU AWEKA WAZI NAMNA ATAKAVYOIENDESHA TAASISI HIYO NYETI YA KUPAMBANA NA WALA RUSHWA NCHINI

soma pia


MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU AWEKA WAZI NAMNA ATAKAVYOIENDESHA TAASISI HIYO NYETI YA KUPAMBANA NA WALA RUSHWA NCHINI

Awaaga Rasmi Watumishi na Wananchi wa Mkoa wa Kagera Kama Katibu Tawala wa Mkoa

Na Sylvester Raphael
Mkurugenzi Mkuu mpya wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) nchini Kamishina wa Polisi Diwani Athumani aongea rasmi na Vyombo vya Habari nchini kwa mara ya kwanza akiwa Mkoani Kagera na kutaja vipaumbele vyake katika kuiongoza TAKUKURU ili iweze kufanya kazi kwa kasi na ufanisi katika mapambano dhidi ya rushwa.

Mkurugenzi Mkuu Diwani Athumani akitaja vipaumbele hivyo Oktoba Mosi, 2018 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kwenye hafla fupi ya kuongea na kuwaaga rasmi Watumishi wa Serikali kama Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera alisema kuwa vipaumbele hivyo vimegawanyika katika sehemu kuu mbili ambapo kuna vipaumbele vya muda mfupi na vya muda mrefu ili kuifanya TAKUKURU kutekeleza majukumu yake kulingana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Vipaumbele vya Muda Mfupi; Kwanza ni kuwasimamia watumishi walio chini ya TAKUKURU kuchapa kazi kwa bidii na kuachana na utendaji wa mazoea. Pili, atahakikisha anachukua hatua stahiki na kwa wakati kwa watumishi wote watakaojihusisha na vitendo vya rushwa. Tatu, Kupeleka Kesi zote za masuala ya rushwa  Mahakamani na kufuatilia mienendo ya kesi hizo. Nne, kufuatilia miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa kama inatekelezwa kwa thamani stahiki kulingana na fedha iliyotolewa na Serikali.

Vipaumbele vya Muda Mrefu: Kwanza, Kufanya uchunguzi katika mfumo wa mapato ili kuziba mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali. Katika kipaumbele hiki Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Diwani Athumani alitolea mfano wa Wafanybiashara wanaotoa risiti za (EFD) zenye gharama pungufu ya kiwango cha fedha tofauti na thamani halisi ya bidhaa ilyonunuliwa kutoka katika maduka yao.

Kipaumbele cha Pili ni kufuatilia kesi zote za rushwa  zilizopo Mahakani na kuhakikisha kesi hizo zinafika mwisho kwa kutolewa hukumu. Tatu, Kutoa elimu kwa umma kuhusu athari za rushwa na kuelimisha wananchi kutojihusisha na vitendo vya rushwa kwani madhara yake ni makubwa. Nne, Kuweka mfumo mzuri wa kuhakikisha wananchi wanatoa taarifa za wala rushwa lakini pia kuhakikisha wananchi hao wanalindwa mara baada ya kutoa taarifa za kweli. Tano, ni kuongeza ushirikiano kati ya TAKUKURU na wadau wote katika mapambano dhidi ya wala rushwa nchini.

Mkurugenzi Mkuu mpya wa (TAKUKURU) nchini Kamishina wa Polisi Diwani Athumani alisema kuwa ameweka vipaumbele hivyo katika kutekeleza majukumu yake akiwa Mkurugenzi Mkuu lengo kuu likiwa ni kumsaidia Rais John Pombe Magufuli katika mapambano dhidi ya rushwa nchini. Lakini pia kuhakikisha anashirikiana na wadau wote wapinga rushwa kuhakikisha kaulimbiu ya “Tanzania Bila Rushwa Inawezekana”  inatimia.
 Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Nchini Kamishina wa Polisi Diwani Athumani akiongea na watumishi wa mkoa wa Kagera wakati wa ziara yake pamoja na kuwaaga.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Mstaafu Marco E Gaguti akitoa shukrani zake kwa  Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Nchini Kamishina wa Polisi Diwani Athumani.
 Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Nesphory  Bwana akitoa neno katika hafla fupi ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kuongea watumishi.
Watumishi wakimsikiliza kwa umakini Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Diwani Athumani
 Baadhi ya waandishi wa habari mkoani Kagera wakiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Diwani Athumani.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU AWEKA WAZI NAMNA ATAKAVYOIENDESHA TAASISI HIYO NYETI YA KUPAMBANA NA WALA RUSHWA NCHINI

yaani makala yote MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU AWEKA WAZI NAMNA ATAKAVYOIENDESHA TAASISI HIYO NYETI YA KUPAMBANA NA WALA RUSHWA NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU AWEKA WAZI NAMNA ATAKAVYOIENDESHA TAASISI HIYO NYETI YA KUPAMBANA NA WALA RUSHWA NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/mkurugenzi-mkuu-wa-takukuru-aweka-wazi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU AWEKA WAZI NAMNA ATAKAVYOIENDESHA TAASISI HIYO NYETI YA KUPAMBANA NA WALA RUSHWA NCHINI"

Post a Comment