title : MBIO ZA ROTARY DAR MARATHON ZAPIGA HODI
kiungo : MBIO ZA ROTARY DAR MARATHON ZAPIGA HODI
MBIO ZA ROTARY DAR MARATHON ZAPIGA HODI
Dar es Salaam. Mwaka huu unaweka alama ya maadhimisho ya miaka 10 ya Mbio za Rotary Dar, tukio la hisani ambalo limekuwa likiweka rekodi kubwa katika usajili kila mwaka.
Kupitia mbio hizo,miradi mbalimbali ya huduma za kijamii imekuwa ikitekelezwa kwa miaka tisa mfululizo iliyopita kupitia fedha ambazo huwa zinachangwa ikiwemo upandaji miti zaidi ya 26,000,utoaji wa huduma ya maji safi ya kunywa shuleni,
Ujenzi wa wodi ya saratani ya watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kituo cha maendeleo ya ujasiriamali Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwaka huu, matembezi ya hisani na mbio za Rotary Dar zinalenga kukusanya fedha kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa kliniki maalum katika Hospitali ya CCRBT itakayowezesha utoaji huduma na kupunguza gharama zinazotolewa kwa watu wenye ulemavu.
Mbio za Rotary Dar ni juhudi za pamoja baina ya klabu nane za Rotary jijini Dar es Salaam ambazo zimekuwa zikiungwa mkono kwa ufadhili mkubwa wa Benki M na Pepsi.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Mwenyekiti wa Bodi wa Mbio za Rotary Dar, Bi. Sharmila Bhatt amesema, "Tunaamini ushirikiano wa kimkakati tuliokuwa nao na Benki M ulikuwa na mafanikio makubwa jambo lilopelekea muelekeo mzuri na kutoa motisha kwa wafadhili wengine katika ambao wanatuunga mkono mwaka huu," alieleza na kuongeza kuwa, "mwaka huu Pepsi nao wameongeza hatua nyingine zaidi kwa ajili ya kutangaza michezo Tanzania kwa kutoa ufadhili wa jumla kwa Mtanzania mwanaume na mwanamke atakayefanya vizuri katika mbio za kilomita 42.2, ambapo watapelekwa kushiriki mbio za Beirut Marathon nchini Lebanon.

Msanii wa kike anayetamba zaidi nchini, Vanessa Mdee al-maarufu Vee-Money ambaye pia ni Balozi wa wa Mbio za Rotary Dar kwa mwaka huu akizungumza leo (Oktoba 02, 2018) jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kutangaza rasmi maandalizi ya mbio za Rotary Dar zitakazofanyika Oktoba 14 mwaka huu (Siku ya Mwalimu Nyerere). Vanessa atashiriki mbio za Rotary Dar kwa mwaka huu lakini pia atatumia ushawishi alionao kuwahamasisha watu wengi zaidi kushiriki. Pamoja nae ni Mwenyekiti wa Bodi wa Mbio za Rotary Dar, Bi. Sharmila Bhatt (kulia) na Mkurugenzi Uendeshaji wa CCBRT, Brenda Msangi (kushoto).
Mkurugenzi Uendeshaji wa CCBRT, Brenda Msangi (kushoto) akionyesha kipeperushi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo (Oktoba 02, 2018) jijini Dar es Salaam kuelezea baadhi ya huduma maalumu zinazotolewa na hospitalini hapo wakati wa hafla ya kutangaza rasmi maandalizi ya mbio za Rotary Dar zitakazofanyika Oktoba 14 mwaka huu (Siku ya Mwalimu Nyerere). Pamoja nae ni Msanii Vanessa Mdee al-maarufu Vee-Money (katikati) ambaye pia ni Balozi wa wa Mbio za Rotary Dar kwa mwaka huu na Mwenyekiti wa Bodi wa Mbio za Rotary Dar, Bi. Sharmila Bhatt (kulia).
Mwenyekiti wa Bodi wa Mbio za Rotary Dar, Bi. Sharmila Bhatt (kulia) akizungumza leo (Oktoba 02, 2018) jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kutangaza rasmi maandalizi ya mbio za Rotary Dar zitakazofanyika Oktoba 14 mwaka huu (Siku ya Mwalimu Nyerere). Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio za Rotary Dar, Catherinerose Barretto, Mkurugenzi Uendeshaji wa CCBRT, Brenda Msangi na Msanii Vanessa Mdee al-maarufu Vee-Money ambaye pia ni Balozi wa wa Mbio za Rotary Dar kwa mwaka huu.
Hivyo makala MBIO ZA ROTARY DAR MARATHON ZAPIGA HODI
yaani makala yote MBIO ZA ROTARY DAR MARATHON ZAPIGA HODI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MBIO ZA ROTARY DAR MARATHON ZAPIGA HODI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/mbio-za-rotary-dar-marathon-zapiga-hodi.html
0 Response to "MBIO ZA ROTARY DAR MARATHON ZAPIGA HODI"
Post a Comment