title : Mapato Sekta ya Madini Yaongezeka Maradufu
kiungo : Mapato Sekta ya Madini Yaongezeka Maradufu
Mapato Sekta ya Madini Yaongezeka Maradufu
Frank Mvungi- MAELEZO
Mapato yanayotokana na madini ya Tanzanite yameongezeka kutoka milioni 166 mwaka 2015 hadi zaidi ya shilingi bilioni 1.28 kwa kipindi cha Januari hadi Septemba 2018.
Akizungumza katika kipindi cha “TUNATEKELEZA” Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki amesema kuwa kuongezeka kwa mapato hayo ni matokeo ya hatua zilizochukuliwa na Serikali ikiwemo ujenzi wa ukuta katika eneo la Mirerani na kuimarishwa kwa ulinzi katika viwanja vya ndege na maeneo yote ya mipakani kuzuia utoroshaji wa madini.
“Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa mchango wa sekta ya madini unaongezeka kutoka asilimia 4.8 kwa sasa hadi kufikia asilimia 10 mwaka 2025;” Alisisitiza Mhe. Kairuki
Akifafanua amesema kuwa Serikali imejipanga kuongeza mapato yanayotokana na madini kwa ujumla kutoka bilioni 301 mwaka 2017/2018 hadi bilioni 310 mwaka 2018/2019.
Aliongeza kuwa katika kuimarisha uwekezaji katika sekta hiyo Wizara ya Madini imendaa makongamano katka nchi za China, Urusi, Israel, India, Thailand, na Falme za Kiarabu ili kuvutia wawekezaji katika sekta ya madini hali itakayosaidia kukuza na kuongeza mchango wake katika pato la Taifa.
Kutokana na marekebisho ya Sheria ya madini yaliyofanyika na kutungwa kwa sheria mpya katika usimamizi wa rasilimali za Taifa kumewezesha mrabaha kuongezeka kutoka asilimia 4 hadi 6 kwa sasa.
Akizungumzia wachimbaji wadogo Mhe. Kairuki amesema kuwa Serikali imewatengea zaidi ya maeneo 46 ili kuwapa fursa ya kushiriki katika ujenzi wa uchumi kupitia katika sekta ya madini.
Pia alieleza kuwa Serikali inawajengea uwezo wachimbaji hao ili waweze kuwa na mbinu za kisasa za uchimbaji, uongezaji thamani na uzingatiaji wa sheria zilizopo kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.
Katika kuimarisha sekta hiyo, Mhe. Kairuki amebainisha kuwa tayari Wizara yake imeanza mchakato wa kuhakikisha kuwa madini ya Tanzanite yanapata hati miliki ikiwa ni utambulisho rasmi kuwa madini hayo yanatoka Tanzania pekee hali itakayoongeza mapato kutokana na madini hayo.
Kipindi cha “TUNATEKELEZA” kinaratibiwa na Idara ya Habari MAELEZO na kurushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania na awamu hii inawashirikisha Waheshimiwa Mawaziri wote.
Hivyo makala Mapato Sekta ya Madini Yaongezeka Maradufu
yaani makala yote Mapato Sekta ya Madini Yaongezeka Maradufu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mapato Sekta ya Madini Yaongezeka Maradufu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/mapato-sekta-ya-madini-yaongezeka.html
0 Response to "Mapato Sekta ya Madini Yaongezeka Maradufu"
Post a Comment