title : MAHAKAMA YAAMURU PEDESHEE NDAMA MTOTO WA NG'OMBE AKAMATWE
kiungo : MAHAKAMA YAAMURU PEDESHEE NDAMA MTOTO WA NG'OMBE AKAMATWE
MAHAKAMA YAAMURU PEDESHEE NDAMA MTOTO WA NG'OMBE AKAMATWE
Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru kukamatwa kwa Mfanyabiashara, Shabani Hussein maarufu kama Pedeshee Ndama mtoto ya Ng'ombe, baada yakushindwa kufika Mahakamani bila kutoa taarifa.
Hati hiyo ya kukamatwa imetolewa leo Oktoba 24.2018 na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Maira Kasonde, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa na mshtakiwa huyo kushindwa kutokea mahakamani.
Aidha Hakimu Maira ametoa barua ya wito kwa wadhamini wa mshtakiwa huyo kufika mahakamani na kueleza alipo mshtakiwa.
Kabla ya kutolewa kwa amri hiyo ya kukamatwa kwa mshtakiwa, wakili wa Serikali, Mosia Kaima, alidai kuwa, kesi hiyo leo imekuja kwa kutajwa lakini mshtakiwa hayupo n ahata mashaidi wake pia hawapo.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 12. 2018 kesi hiyo itakapokuja kwa kutajwa.
Ndama anakabiliwa na mashtaka matano yakiwemo ya kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu,
Mshtakiwa anadaiwa kughushi nyaraka ya kibali cha kusafirisha madini na sampuli za madini kwa kusudi la kuonesha kuwa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited iliruhusiwa kusafirisha maboksi manne ya dhahabu yenye kilogramu 207 yenye thamani ya Dola za Marekani 8,280,000.00 kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited wakati akijua si kweli.
Pia anadaiwa kughushi kwa kutengeneza hati ya kibali ya Umoja wa Mataifa ofisi ya Dar es Salaam akijaribu kuonesha kilogramu 207 za dhahabu kutoka nchini Congo zinatarajiwa kusafirishwa na kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited, zimesafirishwa bila jinai yoyote wakati akijua si kweli.
Hivyo makala MAHAKAMA YAAMURU PEDESHEE NDAMA MTOTO WA NG'OMBE AKAMATWE
yaani makala yote MAHAKAMA YAAMURU PEDESHEE NDAMA MTOTO WA NG'OMBE AKAMATWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA YAAMURU PEDESHEE NDAMA MTOTO WA NG'OMBE AKAMATWE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/mahakama-yaamuru-pedeshee-ndama-mtoto.html
0 Response to "MAHAKAMA YAAMURU PEDESHEE NDAMA MTOTO WA NG'OMBE AKAMATWE"
Post a Comment