KAIMU MKURUGENZI TPA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO

KAIMU MKURUGENZI TPA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KAIMU MKURUGENZI TPA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KAIMU MKURUGENZI TPA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO
kiungo : KAIMU MKURUGENZI TPA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO

soma pia


KAIMU MKURUGENZI TPA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
KAIMU Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa mamlaka ya bandari Tanzania, (TPA) Peter Gawile amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kuisababishia TPA hasara ya zaidi ya sh milioni 150.

Akisomewa hati ya mashtaka na wakili wa serikali kutoka Takukuru, Lizy Kiwia mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi imedaiwa, Oktoba 25, 2012  huko katika ofisi kuu za TPA zilizopo, Temeke mshtakiwa huyo  wakati akijua na kwa nia ya kumdanganya muajiri wake alitumia nyaraka ya malipo ya kodi (Invoice) namba MKOO/722A kutoka Kampuni ya Bob investment Ltd. 

Akidai kuwa, garama ya  semina ya siku tatu ilikuwa ni sh. 47,935,140 wakati akijua alikuwa na lengo La kumdanganya muajiri wake huyo TPA.

Katika shtaka la pili imedaiwa siku na mahali hapo mshtakiwa huyo wakati akijua na kwa nia ya kumdanganya muajiri wake alitumia nyaraka ya malipo ya kodi (Invoice) namba MKOO/722B kutoka Kampuni ya Bob investment Ltd. Akidai kuwa, garama ya  semina ya siku tatu ilikuwa ni sh. 47,935,140 wakati akijua alikuwa na lengo La kumdanganya muajiri wake huyo TPA.

Katika shtaka la tatu mshtakiwa anadaiwa, Desemba 5 2012 akiwa TPA alitumia hati ya malipo namba MKOO/1203 Kutoka huko huko Bob yenye garama ya sh, 97,178,664

Katika shtaka la nne imedaiwa kati ya Oktoba 30 na Desemba 12/2012  huko TPA, mshtakiwa kwa nia ovu aliisababishia TPA hasara ya sh 158,947,584.

Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande kwa Kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo yalimtaka kuwa na wadhamini mawili wenye barua za utambulisho.

Pia, Hakimu alisema mshtakiwa atatakiwa kuweka nusu ya fedha hizo au kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo. Kesi imeahirishwa hadi hadi Oktoba 29, 2018 kwa kutajwa na kuangalia upelelezi umekamilika au la.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa mamlaka ya bandari Tanzania, (TPA) Peter Gawile akiingia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo kujibu mashtaka matatu likiwemo la kuisababishia TPA hasara ya zaidi ya sh milioni 150.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa mamlaka ya bandari Tanzania, (TPA) Peter Gawile akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kujibu mashtaka matatu likiwemo la kuisababishia TPA hasara ya zaidi ya sh milioni 150.


Hivyo makala KAIMU MKURUGENZI TPA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO

yaani makala yote KAIMU MKURUGENZI TPA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KAIMU MKURUGENZI TPA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/kaimu-mkurugenzi-tpa-afikishwa-mahakama.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "KAIMU MKURUGENZI TPA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO"

Post a Comment