JAJI MSTAAFU AWAASA WADAU WA MAHAKAMA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI

JAJI MSTAAFU AWAASA WADAU WA MAHAKAMA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JAJI MSTAAFU AWAASA WADAU WA MAHAKAMA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JAJI MSTAAFU AWAASA WADAU WA MAHAKAMA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI
kiungo : JAJI MSTAAFU AWAASA WADAU WA MAHAKAMA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI

soma pia


JAJI MSTAAFU AWAASA WADAU WA MAHAKAMA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI

Na Karama Kenyunko, globu ya Jamii
JAJI mstaaafu Mahakama Kuu ya Tanzania, Aloycisious Mujulizi amewaasa wadau wa mahakama na wasomi waliopo kwenye tasnia ya sheria kuacha kutumia lugha ya Kingereza pale wanapofanya shughuli zao hasa wakati wa kuandika ushahidi na hukumu badala yake watumie lugha ya kiswahili kwa kuwa inajylikana na watanzania walio wengi.

Jaji Mujuluzi ameyasema hayo leo Oktoba 26.1018 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi ya kuwaaga kitaaaluma majaji saba  wa mahakama kuu waliostaafu wamestaafu. 

Amesema hakuna haja kwa mahakama kutumia lugha ya kingereza kama lugha rasmi ya kunukuu kumbukumbu za mahakama na kuongeza, jambo hilo likiachwa liendelee wananchi wataendelea kuamini kuwa vyombo vya utoaji haki zinakula rushwa wakati si kweli. 

Amesema, kama lugha ya kiingereza ikiachwa iendelee basi wala rushwa watatumia kivuli hicho kuhararisha mambo yao hivyo ili kuondokana na uwepo wa ukalimani mahakamani jaji au Hakimu aandike kwa kiswahili ushahidi wote unaotolewa mahakamani hata hukumu pia lakini anavyopokea neno la kishwahili na kuandika kwa kingereza.

"Lugha ya kiswahili imefanywa kuwa ya taifa lakini pia anaamini lugha nyingine za kienyeji zinapaswa kuendelezwa katika vyuo mbalimbali nchini na kuandikwa kwenye vitabu ili iwasaidie majaji wanaopelekwa mkoani kuweza kusoma vitabu hivyo". Amesema

Ameongeza, kitu kingine kinachowafanya baadhi ya watu kutoiamini mahakama ni pale ushahidi unaotolewa kukutwa umeandikwa tofauti jambo linalochangiwa na majaji kutokuwa na utaalamu wa kuandika kwa ufupi na wingi wa kazi. 

Wote tunafahamu kuwa ukiwa unaandika uwezi kuwa wakati huo huo unamuangalia kwa umakini usoni shahidi anayetoa ushahidi mbele yako  kwahiyo mimi naona hakuna haja ya kutumia kingereza ni vema tuondokana Kabisa.

Naye Jaji Kiongozi Mahakama kuu ya Tanzania,  Dk. Eliezer Feleshi amesema anatambua kuwa yapo maeneo ambayo yanahitaji maboresho hasa mifumo ya kuwezesha usikilizwaji wa kesi.

Amesema mahakama inaendelea na kazi yake ya kufanya maboresho na kwamba ni safari ya muda mrefu ambayo bado wanaendelea nayo kwa kuchukua hatua mbalimbali. Ukiwemo na mpango mkakati wa kumrahisishia jaji au hakimu kuandika hukumu, 

Aidha amesema kupitia kwa majaji wastaafu wamejifunza mambo mengi hasa kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii kwa kufuata misingi ya haki na utawala bora. 
 Jaji kiongozi Elieza Fereshi watatu kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya majaji mara baada ya hafla fupi ya kuwaaga kitaaaluma majaji saba  wa mahakama kuu waliostaafu wamestaafu. 
Jaji kiongozi Elieza Fereshi watatu kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya majaji mara baada ya hafla fupi ya kuwaaga kitaaaluma majaji saba  wa mahakama kuu waliostaafu iliyofanyika leo jijini Dar Es Salaam katika ukumbi wa wazi wa Mahakama Kuu.
Jaji kiongozi Elieza Fereshi akimkabidhi ua jaji mstaaafu Mahakama Kuu ya Tanzania, Aloycisious Mujulizi mara baada ya hafra ya kuwaaga kitaaluma iliyofanyika leo jijini Dar Es Salaam katika ukumbi wa wazi wa Mahakama Kuu.


Hivyo makala JAJI MSTAAFU AWAASA WADAU WA MAHAKAMA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI

yaani makala yote JAJI MSTAAFU AWAASA WADAU WA MAHAKAMA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JAJI MSTAAFU AWAASA WADAU WA MAHAKAMA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/jaji-mstaafu-awaasa-wadau-wa-mahakama.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "JAJI MSTAAFU AWAASA WADAU WA MAHAKAMA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI"

Post a Comment