title : HAWA KUFANYIWA UPASUAJI WA MOYO NCHINI INDIA
kiungo : HAWA KUFANYIWA UPASUAJI WA MOYO NCHINI INDIA
HAWA KUFANYIWA UPASUAJI WA MOYO NCHINI INDIA
Na Khadija Seif, Blobu ya Jamii
Mwanamuziki wa kike nchini anaejulikana kwa jina la Hawa aliyeshirikishwa kwenye wimbo wa nitarejea wa Mwanamuziki Naseeb Abdul 'Diamond platinum' amefanikiwa kupata vipimo vya awali nchini India.
Hawa ambaye hivi karibuni alikua akiomba msaada kwa watu mbalimbali ikiwemo kwa Diamond ili aweze kupata matibabu ya ugonjwa ambao ulikua ukimsumbua muda mrefu huku wengi wakimtupia lawama kuwa amejiingiza Kwenye ulevi wa kupindukia.
Akithibitisha hayo Meneja wa Daimond Platinum, Hamis Tale maarufu kama Babu Tale ameeleza kuwa wamefika salama nchini India na kufanikiwa kupata vipimo vya awali .
Tale ameweka wazi kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa mpaka sasa asilimia 95 inaonyesha kuwa Hawa hana tatizo lolote la ini kama ilivokua ikisemekana hapo awali kutokana na tumbo lake kujaa maji na kupelekea baadhi ya watu kutafsiri hali hiyo ni ugonjwa wa ini
Hivyo basi tale amesema kuwa Hawa amefanya kipimo cha moyo nakugundulika kuwa ndio chanzo kilichokua kikipelekea mwili kujaa maji .
Kwa upande wa Wataalamu wanaendelea kuhakikisha Hawa anapata matibabu na taratibu zinaendelea vizuri ili aweze kufanyiwa upasuaji mkubwa ambao utahitaji uangalizi sana.
Pia Meneja huyo ameshukuru sana juhudi ambazo zinaonyeshwa kwa msanii daimond kwa kumsaidia mwana Dada huyo ili kuhakikisha anarudi katika hali yake ya kawaida na kuwasihi watu kumuombea dua sana katika kipindi hiki.
Hivyo makala HAWA KUFANYIWA UPASUAJI WA MOYO NCHINI INDIA
yaani makala yote HAWA KUFANYIWA UPASUAJI WA MOYO NCHINI INDIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HAWA KUFANYIWA UPASUAJI WA MOYO NCHINI INDIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/hawa-kufanyiwa-upasuaji-wa-moyo-nchini.html
0 Response to "HAWA KUFANYIWA UPASUAJI WA MOYO NCHINI INDIA"
Post a Comment