title : HATIMAYE JIMBO LA LIWALE LAPATA MUWAKILISHI BUNGENI
kiungo : HATIMAYE JIMBO LA LIWALE LAPATA MUWAKILISHI BUNGENI
HATIMAYE JIMBO LA LIWALE LAPATA MUWAKILISHI BUNGENI
Na. Vero Ignatus, Liwale - Lindi
Hatimaye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Liwale umemalizika kwa huku mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM) Zuberi Kuchauka akiibuka mshindi wa kiti cha ubunge
Msimamizi uchaguzi Jimboni hapo Luiza Mlelwa amesema waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 55777 na waliojitokeza kupiga kura walikuwa 40706 kura halali zilikuwa 40,301 kura zilizokataliwa ni 405
Akimtangaza mshindi wa kiti cha ubunge (6:30usiku ) Jimbo la Liwale msimamizi wa uchaguzi amesema kuwa Zuberi ameshinda kwa kura 34, 582 sawa na asilimia 85.81.Mara baada ya kutangazwa mshindi wa kiti cha Ubunge Zuberi Mchauka amesema ameyapokea matokeo kwa furaha na ameahidi kushirikiana na wananchi wa Jimbo la Liwale kutatua changamoto mbalimbali zilizopo
Aidha Mchauka amesema kuwa changamoto nyingi zilizopo katika Jimbo la Liwaleni pamoja na miundombinu ya barabara, maji, Elimu, mawasiliano na Afya ambapo ameahidi wananchi kuwa atashughulikia changamoto hizo.
Abdul Kombo Ngakolwa mgombea wa chama cha (AAFP) chama cha wakulima amesema ameridhishwa na ushindi alioupata mgombea wa(CCM) na amempongeza, kwa ushindi huo '' Mara zote mtu unaposhindana lazima mmoja ashinde, asiyekubali kushindwa siyo mshindani'' alisema Abdul
Mwajuma Notey mgombea kutoka (UMD) amewapongeza wanaliwale kwa kufanya maamuzi yao na amesema anayaheshimu, amempongeza mbunge mteule kwa ushindi huo ."Nakupongeza sana kwa ushindi ila namkumbusha tu awakumbuke wapiga kura wako wote waliomchagua na wasiomchagua wote ni wapigakura wako"
Mchakato wa kumtafuta mbunge wa Jimbo la Liwale ulianza mwezi mmoja uliopita ambapo waliotangaza nia ya kuwania kiti hicho ni wagombea kutoka vyama vifuatavyo AAFP kura 18 sawa 0.2% (UMD 109 sawa 0.49% ACT 285 sawa 0.79%CUF 5207 sawa na 12. 92%.

Wa pili kutoka kulia ni Msimamizi wa Uchaguzi mdogo Jimbo la Liwale Luiza Mlelwa akiniandaa kumtangaza mshindi wa kigi cha ubunge Jimboni hapo.

Mbunge Mteule wa Jimbo la Liwale akionyesha cheti alichokabidhiwa na msimamizi wa uchaguzi mara baada ya kutangazwa rasmi. Picha na Vero Ignatus
Hivyo makala HATIMAYE JIMBO LA LIWALE LAPATA MUWAKILISHI BUNGENI
yaani makala yote HATIMAYE JIMBO LA LIWALE LAPATA MUWAKILISHI BUNGENI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HATIMAYE JIMBO LA LIWALE LAPATA MUWAKILISHI BUNGENI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/hatimaye-jimbo-la-liwale-lapata.html
0 Response to "HATIMAYE JIMBO LA LIWALE LAPATA MUWAKILISHI BUNGENI"
Post a Comment