title : Dr Mengi azindua jengo la Kliniki ya Moyo
kiungo : Dr Mengi azindua jengo la Kliniki ya Moyo
Dr Mengi azindua jengo la Kliniki ya Moyo
Na Mwandishi wetu
Vijana wakijiamini wanaweza kuwa chachu ya maendeleo ya nchi hasa iwapo watakuwa wabunifu wa miradi ya utoaji huduma muhimu za kijamii.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr Reginald Mengi ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akizindua jengo jipya la Kliniki ya HEAMEDA, eneo la Bunju B, inayotibu magonjwa ya moyo, baada ya kutembezwa idara mbalimbali za utoaji huduma wa kliniki hiyo.
Akipongeza uwekezaji mkubwa uliofanywa katika ujenzi na ununuzi wa vifaa tiba, Dr MENGI amesema watu waliofanya maajabu makubwa duniani ni wale wanaojiamini na kuthubutu kutekeleza ndoto zao.
Akizungumza katika hafla hiyo, iliyoambatana na maadhimisho ya miaka minane ya kuanzishwa kwa kliniki hiyo, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Bw. Daniel Chongolo amesema uwekezaji uliofanywa katika kliniki hiyo ni wa kizalendo wenye malengo ya kusaidia wananchi kupata tiba muhimu ya magonjwa ya moyo.
Mapema katika taarifa yake Mkurugenzi Mkuu wa Kliniki ya Heameda Dr. Hery Mwandolela alisema Kiliniki hiyo iliyoanza kutoa huduma kwenye vyumba viwili na watumishi wawili, sasa hivi ina watumishi 30, jengo kubwa lenye vitendea kazi vya kisasa, na hadi sasa imeshawahudumia wagonjwa wapatao 13,000
Aidha Mwakilishi wa Mganga MKUU wa wilaya ya Kinondoni Dr Christowell Mande amepongeza uwekezaji huo na kuahidi kutoa ushirikiano wa karibu.
Mgeni rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr. Reginald Mengi akizindua rasmi jengo jipya la Kliniki HEAMEDA uzinduzi ulioambatana na maadhimisho ya miaka minane ya kuanzishwa kwa kliniki hiyo iliyopo eneo la Bunju B jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kliniki ya HEAMEDA, Dr. Hery Mwandolela pamoja na Mwakilishi wa Mganga MKUU wa wilaya ya Kinondoni Dr Christowell Mande (wa kwanza kushoto) pamoja na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Bw. Daniel Chongolo (katikati kushoto).
Mgeni rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr. Reginald Mengi akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu wa Kliniki ya HEAMEDA, Dr. Hery Mwandolela mara baada ya kuzindua rasmi jengo la kliniki hiyo kwenye hafla iliyoambatana na maadhimisho ya miaka minane ya kuanzishwa kwa kliniki hiyo iliyopo eneo la Bunju B jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr. Reginald Mengi akizungumza na wafanyakazi pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo la kliniki hiyo ulioambatana na maadhimisho ya miaka minane ya kuanzishwa kwa kliniki hiyo iliyopo eneo la Bunju B jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Bw. Daniel Chongolo akitoa salamu kwa niaba ya serikali ambapo aliahidi kushughulikia ukarabati wa barabara inayoelekea kwenye kliniki ya HEAMEDA iliyopo eneo la Bunju B jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la kliniki hiyo ulioambatana na maadhimisho ya miaka minane ya kuanzishwa kwa kliniki hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kliniki ya HEAMEDA, Dr. Hery Mwandolela akitoa taarifa ya HEAMEDA kwa mgeni rasmi na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la kliniki hiyo ulioambatana na maadhimisho ya miaka minane ya kuanzishwa kwa kliniki hiyo iliyopo eneo la Bunju B jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr. Reginald Mengi akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kliniki ya HEAMEDA, Dr. Hery Mwandolela ndani maabara ya kliniki hiyo kuhusu mashine za kisasa wanazotumia kufanya vipimo mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la kliniki hiyo ulioambatana na maadhimisho ya miaka minane ya kuanzishwa kwa kliniki hiyo iliyopo eneo la Bunju B jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr. Reginald Mengi (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa Kliniki ya HEAMEDA, Dr. Hery Mwandolela (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Mganga MKUU wa wilaya ya Kinondoni Dr Christowell Mande (kulia) wakifurahi jambo ndani ya maabara ya kliniki hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la kliniki hiyo ulioambatana na maadhimisho ya miaka minane ya kuanzishwa kwa kliniki hiyo iliyopo eneo la Bunju B jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr. Reginald Mengi akimshauri jambo Mkurugenzi Mkuu wa Kliniki ya HEAMEDA, Dr. Hery Mwandolela wakati akikagua idara mbalimbali za kliniki hiyo kabla ya kuzindua jengo la kliniki hiyo katika hafla iliyoambatana na maadhimisho ya miaka minane ya kuanzishwa kwa kliniki hiyo iliyopo eneo la Bunju B jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mtaalamu wa Mabaara wa Kliniki ya HEAMEDA, Bi. Asha Suleiman.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Dr Mengi azindua jengo la Kliniki ya Moyo
yaani makala yote Dr Mengi azindua jengo la Kliniki ya Moyo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Dr Mengi azindua jengo la Kliniki ya Moyo mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/dr-mengi-azindua-jengo-la-kliniki-ya.html
0 Response to "Dr Mengi azindua jengo la Kliniki ya Moyo"
Post a Comment