DC Mjema aagiza Manispaa ya Ilala Kufanya ukaguzi wa kukagua magorofa .

DC Mjema aagiza Manispaa ya Ilala Kufanya ukaguzi wa kukagua magorofa . - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DC Mjema aagiza Manispaa ya Ilala Kufanya ukaguzi wa kukagua magorofa ., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DC Mjema aagiza Manispaa ya Ilala Kufanya ukaguzi wa kukagua magorofa .
kiungo : DC Mjema aagiza Manispaa ya Ilala Kufanya ukaguzi wa kukagua magorofa .

soma pia


DC Mjema aagiza Manispaa ya Ilala Kufanya ukaguzi wa kukagua magorofa .






Wajumbe wa Kamati ya uchunguzi kuhusiana na jengo la ghorofa kumi lililoko Mtaa wa Mfaume eneo la Upanga Dar es Salam wakiwa katika picha ya pamoja ,wakati wa kukabidhi taarifa ya uchunguzi ya gholofa lililo kuwa liko katika  hatari ya kuporomoka kutokana na hitilafu ya nguzo,Pichani Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akipokea taarifa kutoka kwa Mhandisi Phares Washa.PICHA NA HERI SHABAN


Na Heri shaaban
Mwambawahabari
MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amemwagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala  kufanya ukaguzi wa magorofa ya Ilaĺa.

Mjema alitoa tamko hilo Dar es Salaam wakati akipokea taarifa ya tume aliyounda ya gorofa kumi ,lililopo Mtaa wa Mfaume eneo la Upanga kuwa lipo katika hatari ya kuporomoka kutokana na hitilafu ya nguzo mojawapo katika jengo hilo.


"Namwagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kufanya oparesheni kukagua magorofa yote  ya Ilala kwani magorofa mengine yamejengwa chini ya kiwango na mengine yamejengwa katika viwanja vidogo njia za kupita akuna,hasa  kata ya Upanga ni hatari kiusalama magorofa yake yalivyojengwa.alisema Mjema.

Ameagiza ifanyike oparesheni
Octobar mwaka huu hadi mwezi Desembar  kama gorofa limejengwa kwa kiwango cha chini watu watatolewa na kutoa amri ya kulivunja kwani ameshangazwa na ujenzi holela wa magorofa kata ya Upanga  na eneo la Olimpio .

Ameitaka manispaa hiyo kuwa makini katika utoaji wa vibari pia watoe adhabu kali kwa Wakandarasi wazembe wasiofata taratibu za ujenzi.

Mkuu wa Wilaya Ilala aliunda Kamati ya Uchunguzi iliyoundwa na wataalam kutoka Taasisi mbalimbali za serikali zikiwemo Taasisi ya kupambana na Rushwa Tanzania TAKUKURU, Bodi ya Usajili wa Wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji majenzi,AQRB ,Bodi ya Wasajili wa Wahandisi ERB Bodi ya  Usajili wa Makandarasi CRB,Ofisa Usalama wa Mkoa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala IMC.

Matokeo ya uchunguzi  katika Tume hiyo Manispaa ya Ilala iliidhinisha kujengwa kwa gorofa kumi Septemba  30/2005 kibali namba 35365  na kibali cha nyongeza namba 35231 cha Julai 2007.

Hata hivyo vibali vilimtaka Mmiĺiki kuzingatia vifungu vya kanuni za ujenzi hata hivyo wakati mmiliki anapewa vibali,kanuni zilikuwa zimeshafutwa tangu mwaka 1994 na hapakuwa na kanuni za kusimamia ujenzi mjini mpaka zilipotungwa tena mwaka 2008 kipindi hicho ujenzi wa jengo hilo ulikuwa umeshakamilika.


Alisema kutokana na ukaguzi wa jengo uliofanyika mapendekezo ya kamati imependekeza jengo lifanyiwe maboresho kama yalivyoelekezwa na kampuni ya Ushauri Kihandisi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(BICO kwa kutumia mkandarasi mwenye uwezo chini ya Mhandisi mwenye uwezo  chini ya usimamizi Mhandisi Mshauri mwenye ujuzi na weledi wa mfumo wa ubebaji uzito kwenye jengo kabla halijaanza kutumika tena kwa makazi ya watu.


Pia maboresho hayo yaambatane na kurekebisha mfumo wa maji safi na maji taka katika gorofa la jengo hilo .

Aliagiza Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wafanye tathimini ya ukubwa wa mabadiliko yaliyofanyika  katika jengo hilo ,na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa taratibu kanuni na sheria za nchi.

Aidha ameagiza Bodi ya usajili wa wakandarasi wafanye tathimini wachukue hatua stahiki dhidi ya kampuni ya B H Ladwa limited kwa kujenga jengo chini ya kiwango na kusabisha hitilafu kwenye nguzo za jengo hilo lililohatarisha usalama wa watu na mali zao.



Hivyo makala DC Mjema aagiza Manispaa ya Ilala Kufanya ukaguzi wa kukagua magorofa .

yaani makala yote DC Mjema aagiza Manispaa ya Ilala Kufanya ukaguzi wa kukagua magorofa . Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DC Mjema aagiza Manispaa ya Ilala Kufanya ukaguzi wa kukagua magorofa . mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/dc-mjema-aagiza-manispaa-ya-ilala.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DC Mjema aagiza Manispaa ya Ilala Kufanya ukaguzi wa kukagua magorofa ."

Post a Comment