Dawa ya asili ya 4A9 yapata usajili rasmi

Dawa ya asili ya 4A9 yapata usajili rasmi - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Dawa ya asili ya 4A9 yapata usajili rasmi, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Dawa ya asili ya 4A9 yapata usajili rasmi
kiungo : Dawa ya asili ya 4A9 yapata usajili rasmi

soma pia


Dawa ya asili ya 4A9 yapata usajili rasmi


Hatimaye baraza la tiba asili na tiba mbadala Tanzania limeisajili na kuitambua rasm dawa ya 4 A 9 kwa lengo la kumpa fursa mtafiti T.R. Msigwa kuitangaza dawa hiyo kwa manufaa ya watanzania na Afrika kwa ujumla ambapo zaidi ya vijana 400 wanatarajiwa kupata ajira nchini. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Mtafiti TR Msigwa amesema kitendo cha Baraza hilo kuisajili dawa hiyo kwa namba TZ 17TM 0007 ni faraja kubwa kwa watanzania kwani licha ya kusaidia watanzania kiafya lakini pia itakuwa ni fursa pekee ya kutoa ajira kwa vijana nchini. 
 Amesema mpango wake sasa ni kuhakikisha anatoa ajira kwa Watanzania ambapo atakuwa na mwakilishi mmoja kila wilaya kwa nchi nzima ya Tanzania kitendo ambacho kitasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana hao kuisambaza na kuitangaza dawa hiyo
Amesema dawa hiyo ya 4A9 ambayo inaimarisha kinga ya mwili na kusaidia kutibu kisukari, shinikizo la damu na maradhi mengine nyemelez, baada ya kusajiliwa atahakikisha inasambazwa kila wilaya kwa nchi nzima ya Tanzania na nje ya Tanzaia. 

 TR  Msigwa amesema dawa hiyo baada ya kupata mafanikio makubwa nje ya Tanzania,kwa kupata usajili huo kutasaidia kupata mafaniko zaidi nchini Tanzania, na kuwataka watanzania kumuunga mkono katika juhudi zake za kuhakikisha 4A9 inatambulika na kuisaidia jamii. 

TR Msigwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa kuwatia moyo watanzania katika kuanzisha viwanda ambapo licha ya kuwa na kiwanda kidogo ambacho kinazalisha dawa hiyo ya 4A9 
Amesema kwa sasa ameshanunua eneo la heka mbili wilayani Kibaha mkoa wa Pwanni kwa lengo la kujenga kiwanda kikubwa kitakacho zalisha dawa hiyo na kuongeza ufanisi zaidi.  

 TR Msigwa amesema baada ya kupata usajili huo Oktoba 20 mwaka huu anatarajia kuanza safari ya kuitambulisha dawa hiyo ya 4A9 nchini nzima akianzia Makambako mkoani Iringa,mbeya mtwara, Lindi, Pemba na uguja


Hivyo makala Dawa ya asili ya 4A9 yapata usajili rasmi

yaani makala yote Dawa ya asili ya 4A9 yapata usajili rasmi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Dawa ya asili ya 4A9 yapata usajili rasmi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/dawa-ya-asili-ya-4a9-yapata-usajili.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Dawa ya asili ya 4A9 yapata usajili rasmi"

Post a Comment