title : CWT Kilolo chawazawadia bati walimu wastaafu
kiungo : CWT Kilolo chawazawadia bati walimu wastaafu
CWT Kilolo chawazawadia bati walimu wastaafu
CHAMA cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kimetoa bati 500 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 8.5 kwa mwalimu mstaafu 25 kama sehemu ya kuwaaga na kuwapongeza kwa utumishi bora katika kazi hiyo ya ualimu .
Akikabidhi bati hizo jana wakati wa hafla fupi ya kuwaaga walimu hao mgeni rasmi katika hafla hiyo afisa utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Josephat Kayombo pamoja na kupongeza CWT wilaya ya Kilolo kwa kutambua mchango wa walimu wenzao ambao wamestaafu bado alitoa wito kwa walimu waliopo kazini kuendelea kujituma kufanya kazi hiyo na kujiepusha na utovu wa nidhamu .
Kayombo alisema serikali imeendelea kuwajali watumishi wote wa umma wakiwemo walimu na kuendelea kulipa stahiki zao ambazo wamekuwa wakizidai hivyo ni lazima kwa watumishi hao kutimiza majukumu yao kwa ufanisi na kuepuka kuonyesha utovu wa nidhamu na jeuri pale mwajili ambapo amua kumpangia kituo kipya cha kazi .
" Walimu ni kielelezo tosha kwa jamii na hakuna yeyote anayeweza kujisifu kwa mafanikio yake bila kutambua mchango wa mwalimu hivyo ni vema walimu kwa umuhumu wenu huo kuendelea kulenda heshima yenu kwa kuonyesha nidhamu na kuzingatia kanuni na taratibu za kazi na kujiepusha kuwa na nidhamu mbovu " alisema Kayombo
Pia alisema kwa kuwa serikali imeendelea kuwalipa mafao yao wastaafu ni vema walimu wastaafu kuwa makini na wimbi la matapeli ambao wamekuwa wakizunguka katika vijiji mbali mbali vya wilaya ya Kilolo na kuorodhesha majina ya walimu wastaafu kwa lengo la kuwatapeli mafao yao ya ustaafu .
Alisema kuwa kiasi cha fedha ambacho wanakipata baada ya kustaafu kinaweza kuja kuwa msaada mkubwa kwao mbele ya safari hivyo umakini unahitajika kwa kuwaepuka matapeli hao .
Aidha Kayombo aliwapongeza walimu wastaafu wa wilaya ya Kilolo kwa kustaafu kwa heshima na kuwa katika zoezi la kuhakiki watumishi wenye vyeti feki walimu hao walihakikiwa na hadi wanastaafu hakukuwa na mwalimu hata mmoja aliyekutwa na cheti feki .
Kuhusu uhamisho wa walimu uliofanyika alisema kuwa anasikitishwa na baadhi ya walimu kuonyesha kugoma kuripoti katika kituo alichopangiwa na hadi sasa baadhi yao hawajaripoti popote jambo ambalo wameanza kuwafuatilia walimu hao .
" Kulikuwa na uhamisho wa aina mbili walimu kutoka sekondari kwenda shule za msingi na walimu wa shule za msingi na yalitolewa maelezo kuwa walimu wa shule za msingi wamepungua na sekondari kuna walimu wa masomo ya sanaa ambao walikuwa wamezidi na hawakuwa na kazi yoyote ndipo ilitolewa amri kuwatoa huko na kwenda kufundisha shule za msingi hapo ndipo ilipoleta shida na kuwa walimu wote wamelipwa kila mmoja zaidi ya shilingi 500,000 kwa walimu wote zaidi ya 90 " alisema Kayombo
Kuwa ila bado watu wanakataa kwenda kuripoti kituoni hivyo aliwataka walimu hao kwenda kazini huku malipo mengine wakiendelea kulipwa kwa awamu na Halmashauri ya Kilolo imeendelea kuwalipa walimu hao .
Afisa utumishi wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Joseptah kayombo (kulia) akiwa na viongozi wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Kilolo wakiwakabidhi bati walimu wastaafu 25 kila mmoja bati 20.
Viongozi wa CWT Kilolo (kulia) wakiwakabidhi walimu wastaafu 25 zawadi ya bati 20 kila mmoja .
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala CWT Kilolo chawazawadia bati walimu wastaafu
yaani makala yote CWT Kilolo chawazawadia bati walimu wastaafu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CWT Kilolo chawazawadia bati walimu wastaafu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/cwt-kilolo-chawazawadia-bati-walimu.html
0 Response to "CWT Kilolo chawazawadia bati walimu wastaafu"
Post a Comment