BENKI YA DCB YAPATA FAIDA YA BILIONI I.4

BENKI YA DCB YAPATA FAIDA YA BILIONI I.4 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BENKI YA DCB YAPATA FAIDA YA BILIONI I.4, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BENKI YA DCB YAPATA FAIDA YA BILIONI I.4
kiungo : BENKI YA DCB YAPATA FAIDA YA BILIONI I.4

soma pia


BENKI YA DCB YAPATA FAIDA YA BILIONI I.4

Mkurugenzi wa Fedha Benki ya Biashara ya DCB Zacharia Kapama (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Benki ya Biashara ya DCB imefanikiwa kupata faida ya bilioni I.4 katika kipindi cha robo tatu ya mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Fedha Benki ya Biashara ya DCB Zacharia Kapama, amesema kuwa mafanikio hayo yametokana na juhudi katika kuhakikisha wanatoka katika hasara ya bilioni I.6 waliyopata mwaka wa jana.

Kapama amesema kuwa katika kuelekea mafanikio hayo waliweza kuboresha mfumo wa endeshaji biashara ambapo gharama za uendeshaji zilishuka pamoja na kuanzisha huduma mpya ya kidigital.

"Tulizindua akaunti ya kidigitali (DCB digital Account), DCB kibubu Digital Account, DCB FDR Digital account. Account hizi zinamuwezesha mteja kufungua akaunti na kufanya miamala yote ya kibenki" amesema Kapama.

Kapama ameeleza kuwa ukuaji wa faida umechangiwa na ukuaji wa mikopo ghafi ya wateja kutoka shilingi bilioni 89.3 septemba 20I7 na kufikia bilioni 9I.3 kwa mwezi Septemba mwaka huu.

Amefafanua kuwa ukuaji huo umechangiwa na utoaji wa mikopo, kwani ujumla ya shilingi bilioni 50 zimetolewa hadi kufika mwezi septemba mwaka huu.

Hata hivyo Kapama ameeleza kuwa kumekuwa na ongezeko la wateja kutoka I44,445 mwezi desemba mwaka jana hadi kufikia wateja I57,366 kwa mwezi septemba mwaka huu.

"Mapato halisi ya benki yatokanayo na riba yameimarika katika robo tatu ikilinganishwa na kipindi hicho cha mwaka uliopita" amesema Kapama.

Amesema kuwa ili kuongeza ufanisi benki imeendelea kulinganisha amana aghali zenye unafuu ili kuendana na hali ya amana katika masoko ya kibenki ambapo amana za wateja zimepungua.

Mkurugenzi wa Biashara Benki ya DCB James Ngaluko, amesema kuwa benki  imeendelea kutengeneza mazingira rafiki kwa water katika kutoa huduma bora.

Ngaluko amesema kuwa kwa sasa wamefanikiwa kupunguza kiwango cha mikopo chechefu kutoka asilimia I8.9 na kufika asilimia I7.8 kwa mwaka huu.

"Upunguaji huu umechangiwa na ongezeko la ufanisi katika ukusanyaji wa madeni, utoaji wa mikopo kwa riba nafuu na kuboreshwa kwa huduma kwa wateja" amesema Ngaluko.





Hivyo makala BENKI YA DCB YAPATA FAIDA YA BILIONI I.4

yaani makala yote BENKI YA DCB YAPATA FAIDA YA BILIONI I.4 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BENKI YA DCB YAPATA FAIDA YA BILIONI I.4 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/benki-ya-dcb-yapata-faida-ya-bilioni-i4.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "BENKI YA DCB YAPATA FAIDA YA BILIONI I.4"

Post a Comment