title : AFISA ELIMU MSINGI MANISPAA YA ILALA AKUTANA ALIMU 3,800 KUTATUA KERO ZAO.
kiungo : AFISA ELIMU MSINGI MANISPAA YA ILALA AKUTANA ALIMU 3,800 KUTATUA KERO ZAO.
AFISA ELIMU MSINGI MANISPAA YA ILALA AKUTANA ALIMU 3,800 KUTATUA KERO ZAO.
Afisa wa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala Elizabeth Thomas akizungumza na walimu wa shule za Msingi Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Walimu wa Shule za Msingi Manispaa ya Ilala wakiwa katika kikao na Afisa wa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala Elizabeth Thomas.
Walimu wa shule za Msingi Manispaa ya ilala wakiwa katika kikao leo jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Walimu wa shule za msingi Manispaa ya Ilala wametakiwa kufata kanuni na taratibu katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo katika sekta ya elimu.
Akizungumza na walimu wa shule za msingi Manispaa ya Ilala leo jijini Dar es Salaam, Afisa wa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala Elizabeth Thomas, amesema kuwa walimu wanapaswa kufanya kazi kwa bidii jambo ambalo litasaidia wanafunzi kupata elimu bora.
Thomas amesema kuwa walimu wakifanya kazi kwa ufanisi sekta ya elimu katika manispaa ya ilala itaendelea kuwa na mafanikio makubwa.
"Umoja na ushirikiano ni sehemu ya kufanikisha utendaji bora, walimu wakiwa bora na wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo yao" amesema Thomas.
Thomas amesema kuwa lengo la kukutana na walimu 3,800 wa shule za msingi katika manispaa ya ilala ni kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili walimu.
Ameeleza kuwa walimu wana kero mbalimbali ambazo zinaendelewa kufanyiwa kazi jambo ambalo linasaidia kuboresha sekta ya elimu katika Manispaa ya ilala.
"Changamoto za walimu ni ndogo ndogo ambazo zinapatiwa majibu, na kila mwaka uwa nakutana na walimu wote wa shule za msingi manispaa ya ilala ili waweze kuniambia kero zao" amesema Thomas.
Katika hatua nyengine Bi Thomas amebainisha kuwa kuna wimbi kubwa la walimu hawafundishi badala yake wamekuwa wakitumia muda wao kwenda halmashauri bila kuwa na sababu ya Msingi.
Amesema kuwa baadhi ya walimu wamekuwa na safari nyingi kitu ambacho sio kizuri kutokana wanafunzi wanakosa walimu wa kuwafundisha.
"Uongozi wa sasa unataka kila mtumishi afanye kazi kwa ufanisi jamba ambalo litasaidia kufika malengo ambayo yamekusudiwa" amesema Bi Thomas
Afisa Utumishi Elimu Msingi Manispaa ya Ilala Rwechungura Beebwa, amesema kuwa walimu wanatakiwa kutumia busara pamoja na kuwa na subira kipindi ambacho wanasubiria mishahara yao.
Amesema kuwa kila jambo linafanywa kwa utaratibu maalumu, wakati ukifika kila mwalimu atapata haki yake kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.
"Kuna walimu wanakwenda kusoma bila kutoa taarifa, ni busara kufata taratibu jambo ambalo chachu ya maendeleo" amesema Beebwa.
Kaimu Katibu Msaidizi Tume ya Utumishi wa Walimu Ilala (TSC) Subira Mwakibete, amesema kuwa kila mwalimu anatamani kupa cheo kulingana elimu aliyokuwa nayo.
Mwakibete amesema kuwa licha ya kutamani huku kupanda daraja lakini kumekuwa na utaratibu maalumu ambao umekuwa ukitumika.
Ameeleza kuwa kuna sababu nyingi ambazo wakati mwengine mtu wanashindwa kupata cheo kwa wakati ikiwemo kukosea kutaja taarifa zake wakati wa kujaza fomu.
"Naomba tuwe na subira wakati tunaendelea kutatua changamoto zenu, kwani kuna baadhi wamekuwa wakikosea tajaza taarifa muhimu" amesema Mwakibete.
Kwa upande wao walimu wa shule za Msingi Manispaa ya Ilala wameonekana kuwa furaha baada ya Afisa wa elimu Msingi akiwa na timu yake kukutana na walimu hao kwa ajili ya kusikiliza kero zao na kuzitatua.
Walimu hao wamebainisha kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili katika utendaji wao ni pamoja na kuchelewa kupandishwa madaraja na malimbukizi ya mishahara.
Mwalimu wa Shule ya Msingi Kichangani Lucy William, amesema kuwa ujio wa Afisa Elimu Msingi ni mzuri kutokana wamekuwa kusikiliza kero zao.
Amesema kuwa bila changamoto zao zinakwenda kupatiwa majibu kwa wakati kitu ambacho kitawapa hamasa ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii.
Hivyo makala AFISA ELIMU MSINGI MANISPAA YA ILALA AKUTANA ALIMU 3,800 KUTATUA KERO ZAO.
yaani makala yote AFISA ELIMU MSINGI MANISPAA YA ILALA AKUTANA ALIMU 3,800 KUTATUA KERO ZAO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AFISA ELIMU MSINGI MANISPAA YA ILALA AKUTANA ALIMU 3,800 KUTATUA KERO ZAO. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/afisa-elimu-msingi-manispaa-ya-ilala.html
0 Response to "AFISA ELIMU MSINGI MANISPAA YA ILALA AKUTANA ALIMU 3,800 KUTATUA KERO ZAO."
Post a Comment