ACACIA kukusanya milioni 340 kuboresha elimu nchini

ACACIA kukusanya milioni 340 kuboresha elimu nchini - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ACACIA kukusanya milioni 340 kuboresha elimu nchini, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ACACIA kukusanya milioni 340 kuboresha elimu nchini
kiungo : ACACIA kukusanya milioni 340 kuboresha elimu nchini

soma pia


ACACIA kukusanya milioni 340 kuboresha elimu nchini

Kampuni ya uchimbaji wa madini Tanzania – Acacia inatarajia kukusanya zaidi ya Sh milioni 340 kwa kupitia mashindano ya mbio za baiskeli kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa elimu kwa jamii zinazozunguka migodi yetu katika kanda ya ziwa. 

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo nchini, Asa Mwaipopo, Meneja Uboreshaji tija kutoka Kampuni ya uchimbaji wa madini nchini Tanzania – ACACIA, Janeth Ruben alisema mashindano hayo wameyapatia jina la ‘Acacia Imara Pamoja Cycle Challenge’ na yanaenda sambamba na mpango wa kampuni wa kujenga jamii endelevu. 

Alisema mpango huo unaofahamika kwa jina la ‘CanEducate’,unatoa kipaumbele katika kuhakikisha jamii zetu – hasa watoto wa kike - wanapata elimu bora kama njia moja wapo ya kujikwamua na umaskini na kufanikisha dhamira ya serikali ya kuinua uchumi na hali za maisha ya watanzania kama ilivyoainishwa kwenye Dira ya Maendeleo 2025. 

“Fedha hizo zitasaidia wanafunzi wanaotoka katika familia maskini na wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwapatia sare na vifaa vingine vya shule ikiwemo vitabu na vifaa mbalimbali. “Pia zitaelekezwa katika kusaidia wanafunzi wa kidato cha tano na sita wanaotoka kwenye maeneo yanayozunguka migodi yetu kwa kuwalipia ada za mitihani, gharama za malazi na usafiri. Wanafunzi wengi wa ngazi hii husafiri umbali mrefu kufika shule zinazotoa elimu kwa ngazi hiyo ya ‘A Level’.” Alisema. 

Ali hasa sasa mpango huo wa CanEducate ulioanza mwaka 2011, umetumia kiasi cha Sh milioni 494 kwa kuwadhamini wanafunzi 3936, na kuziwezesha kwa njia mbalimbali shule zaidi ya tisa. 

Meneja Uboreshaji tija kutoka Kampuni ya uchimbaji wa madini nchini Tanzania – ACACIA, Janeth Ruben (katikati), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu wa mashindano ya mbio za baiskeli zinazojulikana kwa jina la ‘Imara Pamoja Cycle Challenge’. Kulia ni Mshauri Mkuu wa Kitengo cha Jamii endelevu – ACACIA, Siama Paul na kushoto ni Rais wa Chama cha Baiskeli Tanzania, Godfrey Mhagama.
Meneja Uboreshaji tija kutoka Kampuni ya uchimbaji wa madini nchini Tanzania – ACACIA, Janeth Ruben (katikati), kulia kwake ni Mshauri Mkuu wa Kitengo cha Jamii endelevu – ACACIA, Siama Paul na kushoto ni Rais wa Chama cha Baiskeli Tanzania, Godfrey Mhagama wakiwa na baadhi ya wanufaika wa mpango wa uwezeshaji wanafunzi wasio na uwezo wa kumudu gharama za elimu ‘CanEducate’. Kampuni hiyo inatarajia kuzindua mbio za baiskeli zinazojulikana kwa jina la ACACIA Imara pamoja kwa lengo la kukusanya fedha za kuboresha sekta ya elimu nchini.
Meneja Uboreshaji tija kutoka Kampuni ya uchimbaji wa madini nchini Tanzania – ACACIA, Janeth Ruben (katikati), kulia kwake ni Mshauri Mkuu wa Kitengo cha Jamii endelevu – ACACIA, Siama Paul, wakimsikiliza mmoja wa wanufaika wa mpango wa kuwawezesha wanafunzi wasio na uwezo wa kumuda gharama za elimu – CanEducate, Jeremiah Nambali ambaye ambehitimu Shahada ya uhandisi wa madini katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya kuwezeshwa na mpango huo unaoratibiwa na Kampuni ya ACACIA kwa kushirikiana na taasisi ya CanEducate. 



Hivyo makala ACACIA kukusanya milioni 340 kuboresha elimu nchini

yaani makala yote ACACIA kukusanya milioni 340 kuboresha elimu nchini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ACACIA kukusanya milioni 340 kuboresha elimu nchini mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/acacia-kukusanya-milioni-340-kuboresha.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "ACACIA kukusanya milioni 340 kuboresha elimu nchini"

Post a Comment