WAZIRI TIZEBA AAGIZA MAKAMPUNI YA MBEGU KUWEKA BEI ELEKEZI

WAZIRI TIZEBA AAGIZA MAKAMPUNI YA MBEGU KUWEKA BEI ELEKEZI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI TIZEBA AAGIZA MAKAMPUNI YA MBEGU KUWEKA BEI ELEKEZI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI TIZEBA AAGIZA MAKAMPUNI YA MBEGU KUWEKA BEI ELEKEZI
kiungo : WAZIRI TIZEBA AAGIZA MAKAMPUNI YA MBEGU KUWEKA BEI ELEKEZI

soma pia


WAZIRI TIZEBA AAGIZA MAKAMPUNI YA MBEGU KUWEKA BEI ELEKEZI

Na Wankyo Gati, Arusha

Waziri wa kilimo, Charles Tizeba ameagiza wadau wa pembejeo nchini kuhakikisha wanaweka bei elekezi  ya mbegu katika vifungashio vya mbegu hizo ili kuwawezesha wakulima wasilanguliwe. Hayo ameyasema leo  wakati akifungua mkutano wa wadau wa mbegu uliolenga kupashana taarifa kuhusu maendeleo ya sekta ya mbegu katika kuhakikisha wanazalisha mbegu nyingi na zenye ubora hapa nchini. 

 Waziri Tizeba alisema kuwa , ni lazima vifungashio vyote vya mbegu viwekwe bei elekezi ili kuzuia watu wanaofanya ulanguzi na kusababisha wananchi kushindwa kununua kutokana na bei kubwa wanayotajiwa.

 "naombeni Sana kila kifungashio kitakachokuwa kimebeba mbegu kiwe na bei elekezi na naagiza kuundwa kwa kamati ya pamoja ya kufuatilia mfumo wa uzalishaji na hizo bei elekezi kwenye vifungashio vyote. "alisema Tizeba.

 Aidha Tizeba pia aliyataka makampuni ya mbegu yanayozalisha mbegu  nje ya nchi na kuuza hapa nchini kuzalisha mbegu hizo hapa hapa nchini ili kuongeza ajira na kuwezesha kulipa kodi na tozo zingine. Alisema kuwa, endapo makampuni hayo yatazalisha mbegu hapa nchini itasaidia mbegu hizo kupatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu huku kukiongeza upatikanaji wa ajira katika sekta hiyo.

 Kwa upande wa Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI) Patrick Ngwediagi aliwataka wafanyabiashara kupunguza uingizaji wa mbegu toka nje bali wazalishe hapa hapa nchini.

 Aliwataka wafanyabiashara wa mbegu kuhakikisha mbegu zao zinakuwa na lebo ya ubora wa taasisi ya Tosci, kinyume cha hapo mbegu hizo zinakuwa ni feki na hivyo wakulima hawatanunua.

 Kwa upande wa Mkurugenzi wa chama cha wazalisha mbegu Tanzania (TASTA), Bob Shuma alisema kuwa, uagizwaji wa mbegu kutoka nje ya nchi una gharama kubwa Sana kutokana na kodi nyingi zinazotozwa hadi kufika hapa, hivyo endapo uzalishaji huo utafanyika hapa utapunguza gharama hizo huku wakulima wakipewa Kwa bei nafuu .


Hivyo makala WAZIRI TIZEBA AAGIZA MAKAMPUNI YA MBEGU KUWEKA BEI ELEKEZI

yaani makala yote WAZIRI TIZEBA AAGIZA MAKAMPUNI YA MBEGU KUWEKA BEI ELEKEZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI TIZEBA AAGIZA MAKAMPUNI YA MBEGU KUWEKA BEI ELEKEZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/waziri-tizeba-aagiza-makampuni-ya-mbegu.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI TIZEBA AAGIZA MAKAMPUNI YA MBEGU KUWEKA BEI ELEKEZI"

Post a Comment