title : Taratibu Mpya za Kusimamia Uagizaji wa Sukari Kukamilika Oktoba - Mwijage
kiungo : Taratibu Mpya za Kusimamia Uagizaji wa Sukari Kukamilika Oktoba - Mwijage
Taratibu Mpya za Kusimamia Uagizaji wa Sukari Kukamilika Oktoba - Mwijage
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Serikali imepanga kukamilisha utaratibu mpya wa kuagiza sukari nchini ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu. Utaratibu huo mpya unatagemewa kuwa mwarobaini wa kukomesha mrundikano wa sukari kwenye viwanda vya sukari nchini.
Hakikisho hilo limetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, mheshimiwa Charles Mwijage wakati akiwasilisha taarifa ya hali ya sukari nchini.
Waziri Mwijage ameliambia bunge kuwa sukari inayozalishwa nchini haikidhi mahitaji na kwa mwaka 2018/19 uzalishaji unakadiriwa kufikia tani 353,651 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na hakuna kiwanda kinachozalisha sukari kwa ajili ya matumizi ya viwandani.
Upungufu huo wa sukari inayozalishwa nchini umesababisha nakisi ya sukari takribani tani 316,349, tani 161,349 zikiwa za matumizi ya kawaida na tani 155,000 kwa ajili ya matumizi ya viwandani.
"Hadi kufikia Septemba 5, 2018, viwanda vyetu vilizalisha jumla ya tani 119,671.19 ambazo ni sawa na asilimia 33.84 ya malengo ya uzalishaji wa sukari kwa mwaka huu hivyo kiasi cha sukari kilichopo nchini kinatosheleza mahitaji ya sukari kwa kipindi cha miezi mitatu mbali na uzalishaji unaoendelea" alisema Mhe. Mwijage.
kulipatia ufumbuzi tatizo hilo Waziri Mwijage amesema Serikali imeshatoa maelekezo kwa wamiliki wa viwanda vya sukari nchini kuwasilisha mapendekezo kuboresha mfumo wa usambazaji ili kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa hiyo muhimu unakuwa wa uhakika na bei nafuu.
Akiongea kuhusu bei na upatikanaji wa sukari, Waziri Mwijage amesema tathmini ya miezi sita kuanzia mwezi Machi hadi Agosti, 2018 inaonyesha hali ya upatikanaji wa bidhaa hiyo ni mzuri na bei yake imekuwa ikitengemaa. Kwenye tathmini hiyo ongezeko la bei limekuwa kati ya shilingi 50 hadi shilingi 150.
Mahitaji ya sukari nchini kwa mwaka yanakadiriwa kuwa tani 670,000 ambapo tani 515,000 ni matumizi ya kawaida na tani 155,000 ni kwa mtumizi ya viwandani.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiwasilisha taarifa ya hali ya Sukari nchini wakati wa mkutano wa 12 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kikao cha nane leo Jijini Dodoma.
Hivyo makala Taratibu Mpya za Kusimamia Uagizaji wa Sukari Kukamilika Oktoba - Mwijage
yaani makala yote Taratibu Mpya za Kusimamia Uagizaji wa Sukari Kukamilika Oktoba - Mwijage Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Taratibu Mpya za Kusimamia Uagizaji wa Sukari Kukamilika Oktoba - Mwijage mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/taratibu-mpya-za-kusimamia-uagizaji-wa.html
0 Response to "Taratibu Mpya za Kusimamia Uagizaji wa Sukari Kukamilika Oktoba - Mwijage"
Post a Comment