WAZIRI MKUU MAJALIWA: WANAJIOSAYANSI MNA WAJIBU WA KULINDA MADINI YETU

WAZIRI MKUU MAJALIWA: WANAJIOSAYANSI MNA WAJIBU WA KULINDA MADINI YETU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU MAJALIWA: WANAJIOSAYANSI MNA WAJIBU WA KULINDA MADINI YETU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU MAJALIWA: WANAJIOSAYANSI MNA WAJIBU WA KULINDA MADINI YETU
kiungo : WAZIRI MKUU MAJALIWA: WANAJIOSAYANSI MNA WAJIBU WA KULINDA MADINI YETU

soma pia


WAZIRI MKUU MAJALIWA: WANAJIOSAYANSI MNA WAJIBU WA KULINDA MADINI YETU

*Ataka waisaidie Serikali kubaini vyanzo vya maji vya uhakika

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wanajiosayansi nchini wawe walinzi wa kwanza wa rasilmali za madini, maji na mafuta bila kujali wako serikalini au kwenye sekta binafsi.

“Katika utendaji wenu wa kazi, mnapaswa kuwa wa kwanza kujua kinachoendelea katika sekta zote mnazohusiana nazo, yaani madini, maji na mafuta. Haijalishi unafanya kazi serikalini au shirika binafsi, wewe ni Mtanzania na una jukumu la kulinda rasilimali za nchi yako.” amesema.

Waziri Mkuu ametoa wito huo leo mchana (Alhamisi, Septemba 27, 2018), wakati akifungua warsha ya siku sita ya Jumuiya ya Wanajiosayansi Tanzania iliyoanza leo kwenye hoteli ya New Dodoma, jijini Dodoma.

Waziri Mkuu ambaye amefungua warsha hiyo kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka wanajiosayansi hao kutoka Serikalini, taasisi binafsi na vyuo vya elimu ya juu wasishiriki kulihujumu Taifa kwani kwa kufanya hivyo, watakuwa wasaliti namba moja.

“Msijihusishe au kushiriki kulihujumu Taifa lenu kwani kwa kufanya hivyo, mtakuwa wasaliti namba moja. Hakikisheni mnakuwa mabalozi wa Serikali katika mashirika haya kwa kutoa elimu juu ya sheria zinazosimamia sekta hizi huku mkisisitiza umuhimu wa kufuata sheria za nchi zenye kusimamia rasilimali zetu adhimu,” amesema.

Amesema mbali ya kilimo, rasilmali miamba na madini ndivyo vyenye mchango mkubwa wa kukuza viwanda kote duniani na kwamba utaalamu wa jiosayansi una mchango mkubwa kwenye malighafi za viwandani, upatikanaji wa maji ya kutosha nchini, mafuta, gesi asilia na uzalishaji wa nishati kupitia jotoardhi.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka wanajiosayansi hao waisaidie Serikali kutafuta vyanzo vya maji vya uhakika ili itumie kihalali fedha zinazotengwa kwenye uchimbaji visima vya maji na kuepuka upotevu wa fedha.

“Ni jukumu la wanajiolojia la kutuambia wapi maji yapatikana. Muandae utaratibu mzuri wa kutunza takwimu kuhusu kiwango cha maji, ni wapi maji yalipo na ujazo wake. Kwenye eneo hili tumepoteza fedha nyingi sana, tumepeleka fedha nyingi kwenye halmashauri ili tutoe huduma za maji wananchi lakini kwa sababu hatukuwashirikisha wanajiosayansi, wachimbaji wameenda kuchimba visima na wakakosa maji, yakabaki mashimo tu bila maji. Mna jukumu kubwa la kuisadia Serikali ili itumie vizuri fedha inazozitenga kwa ajili ya maji kwa kubainisha wapi kuna maji, yako kiasi gani na yako umbali gani,” amesema.

Wakati huohuo, Waziri wa Madini, Bibi Angella Kairuki amesema wizara hiyo inakusudia kuanzisha chombo maalum cha usajili cha kuwatambua wanajiosayansi kisheria kupitia Bodi ya Usajili wa Wanajiosayansi nchini (Geoscientists Registration Board -GRB) kama ilivyo kwa wahasibu, wahandisi na mabaraza ya wasajili mbalimbali ili kukabiliana na wataalamu feki wa fani hiyo.

“Wizara ya Madini inategemea wanajiosayansi wawe wazalendo kwa Taifa kwa kutoa taarifa za kitaalamu zinazoendama na uhalisia ili kuondoa malalamiko yanayotokana na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu hasa wale wanaojifanya wataalamu ilhali wakijua wazi hawana utaalamu wa fani hii,” amesema.

Amesema azma ya Serikali ni kumaliza changamoto zinazoikabili sekta hiyo ya madini zikiwemo ukiritimba uliokuwa ukifanyika katika mlolongo mzima wa utoaji leseni, utafutaji na uzalishaji wa rasilmali madini.
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa mwananjiolojia, Batwenge Chakutema kuhusu vifaa mbaIimbali vinavyotumika katika utafiti na upimaji madini wakati alipofungua Warsha  ya Jumuiya ya Wanajiosayansi Tanzania  (Tanzania  Geological Society - TGS) kwenye hoteli ya New Dodoma, Septemba 27, 2018 . 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akifungua Warsha   ya Jumuiya ya Wanajiosayansi Tanzania  (Tanzania  Geological Society - TGS) kwenye hoteli ya New Dodoma, Septemba 27, 2018
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia zawadi ya kinyago cha njiwa wawili kilichotokana na jiwe  wakati  alifungua  Warsha  ya Jumuiya ya Wanajiosayansi Tanzania  (Tanzania  Geological Society - TGS) kwenye hoteli ya New Dodoma, Septemba 27, 2018 . Kushoto ni Waziri wa Nishati, Angela Kairuki na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas  Katambi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Warsha  ya Jumuiya ya Wanajiosayansi Tanzania  (Tanzania  Geological Society - TGS) kwenye hoteli ya New Dodoma, Septemba 27, 2018 . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Hivyo makala WAZIRI MKUU MAJALIWA: WANAJIOSAYANSI MNA WAJIBU WA KULINDA MADINI YETU

yaani makala yote WAZIRI MKUU MAJALIWA: WANAJIOSAYANSI MNA WAJIBU WA KULINDA MADINI YETU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU MAJALIWA: WANAJIOSAYANSI MNA WAJIBU WA KULINDA MADINI YETU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/waziri-mkuu-majaliwa-wanajiosayansi-mna.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI MKUU MAJALIWA: WANAJIOSAYANSI MNA WAJIBU WA KULINDA MADINI YETU"

Post a Comment