WAZIRI MKUU ATAKA MIKAKATI ZAIDI KUKABILIANA NA DAWA ZA KULEVYA

WAZIRI MKUU ATAKA MIKAKATI ZAIDI KUKABILIANA NA DAWA ZA KULEVYA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU ATAKA MIKAKATI ZAIDI KUKABILIANA NA DAWA ZA KULEVYA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU ATAKA MIKAKATI ZAIDI KUKABILIANA NA DAWA ZA KULEVYA
kiungo : WAZIRI MKUU ATAKA MIKAKATI ZAIDI KUKABILIANA NA DAWA ZA KULEVYA

soma pia


WAZIRI MKUU ATAKA MIKAKATI ZAIDI KUKABILIANA NA DAWA ZA KULEVYA

*Azungumzia dawa za viwandani zinavyotumika kama dawa za kulevya

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAZIRI MKUUKassim Majaliwa amesema matumizi ya dawa za kulevya nchini yamepungua kwa asilimia 90 huku akieleza kuwepo kwa mbinu mpya ambapo dawa za viwandani zimeanza kutumiwa na baadhi ya watu kama sehemu dawa za kulevya.


Hivyo amesema ipo haja ya kuhakikisha kunakuwa na mikakati mipya ya kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya huku akiomba wakuu wa vyombo vinavyohusika na kukabiliana na matumizi ya dawa za kulevya barani Afrika kuweka mikakati ya kuiabiliana na mbinu mbalimbali ambazo zinatumiwa na wanaofanya biashara hiyo.

Waziri Mkuu amesema hayo leo baada ya kufungua mkutano wa 28 wa wakuu wa vyombo vinavyopambana na dawa za kulevya kutoka nchi za Afrika ujulikanao kama (28th HONLEA- Afrika), jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere(JNICC),ambao unashirikisha wajumbe zaidi ya 120 kutoka nchi 54 za Afrika.

Hivyo ametumia nafasi hiyo kueleza ipo haja kwa nchi hizo kuangalia kwa namna gani wanaweza kuweka mikakati ya kukomesha biashara ya dawa za kulevya.
Ameeleza namna ambavyo baada ya kufanikiwa kudhibitiwa kwa dawa za kulevya wapo baadhi ya watu wasiwaaminifu ambao wanachukua dawa zinazotengenezwa viwandani kama sehemu ya dawa za kulevya.


Ametoa mfano wa dawa hizo ni pamoja na dawa za usingizi ."Zipo dawa zinazotengenezwa viwandani watu wasiowaaminifu wanazichukua na kisha kuzibadilishia matumizi kuwa dawa za kulevya,"amesema.

Hivyo amesema lengo la  mkutano huo ni kubadilishana uzoefu na kupanga mikakati ya pamoja kuhusu udhibiti na mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya katika nchi hizo.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Vyombo Vinavyopambana na Biashara ya Dawa za Kulevya   kutoka nchi za Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC)  jijini Dar es salaam Septemba 17, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Bibi Jo Dedeyne ambaye ni  Katibu Mkuu Kiongozi wa Taasisi za  Umoja wa Mataifa zinazoshughulikia dawa za kulevya na uhalifu (United Nations Office on Drugs na Crime - UNODC)  baada ya kufungua Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Vyombo vinavyopambana na Dawa za Kulevya   kutoka nchi za Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Septemba 17, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala WAZIRI MKUU ATAKA MIKAKATI ZAIDI KUKABILIANA NA DAWA ZA KULEVYA

yaani makala yote WAZIRI MKUU ATAKA MIKAKATI ZAIDI KUKABILIANA NA DAWA ZA KULEVYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU ATAKA MIKAKATI ZAIDI KUKABILIANA NA DAWA ZA KULEVYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/waziri-mkuu-ataka-mikakati-zaidi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI MKUU ATAKA MIKAKATI ZAIDI KUKABILIANA NA DAWA ZA KULEVYA"

Post a Comment