WANANCHI WILAYANI BARIADI WARIDHIA KUACHIA MAENEO YAO KUPISHA UJENZI WA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA SIMIYU

WANANCHI WILAYANI BARIADI WARIDHIA KUACHIA MAENEO YAO KUPISHA UJENZI WA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA SIMIYU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WANANCHI WILAYANI BARIADI WARIDHIA KUACHIA MAENEO YAO KUPISHA UJENZI WA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA SIMIYU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WANANCHI WILAYANI BARIADI WARIDHIA KUACHIA MAENEO YAO KUPISHA UJENZI WA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA SIMIYU
kiungo : WANANCHI WILAYANI BARIADI WARIDHIA KUACHIA MAENEO YAO KUPISHA UJENZI WA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA SIMIYU

soma pia


WANANCHI WILAYANI BARIADI WARIDHIA KUACHIA MAENEO YAO KUPISHA UJENZI WA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA SIMIYU

Na Stella Kalinga, Simiyu 

Wananchi wa Vijiji vya Igegu na Nga’arita Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi wameridhia kuachia maeneo yao kupisha Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Mkoani Simiyu ambacho kinatarajiwa kujengwa katika eneo la Igegu wilayani .

Wananchi hao wameyasema hayo Septemba 14, 2018 wakati wa uzinduzi wa zoezi la Uthamini na upimaji wa maeneo hayo, ambalo linatarajiwa kumalizika baada ya mwezi mmoja na wiki mbili kuanzia sasa.

Wamesema kuwa wamefurahishwa na hatua ya Serikali kujenga Kiwanja cha Ndege wilayani Bariadi na kwa kuwa ujenzi huo ni suala la maendeleo hawawezi kupinga, huku wakiiomba Serikali kuhakikisha wanalipa fedha za fidia kwa wakati mara tu baada ya kukamilisha zoezi la uthamini na upimaji wa maeneo hayo.

“Kwa kuwa ujenzi wa kiwanja cha ndege ni maendeleo hatuwezi kukataa kutoa maeneo yetu, tumekubali kutoa maeneo ila ombi letu kwa Serikali tunaomba tulipwe fidia ya maeneo yetu kwa wakati na tulipwe kwa haki” alisema Ndaturu Malemi mkazi wa Kijiji cha Igegu.

“Tumekubali kutoa maeneo yetu Uwanja wa Ndege ujengwe, ushauri wangu tu ni kwamba kwa kuwa tunaelekea msimu wa kuandaa mashamba baada ya tathmini tunaomba tuliokuwa na maeneo hapa tuambiwe mapema kama ujenzi utaanza au tunaweza kuendelea na shughuli za kilimo”alisema Mahembe Mayumba mkazi wa Kijiji cha Igegu
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ng’arika Kata ya Sapiwi Septemba 14, 2018 wilayani humo, katika Uzinduzi wa zoezi la uthamini na upimaji wa maeneo ambayo Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Simiyu kitakapojengwa . 
Meneja wa Kiwanja cha Ndege Shinyanga Bi.Beaster Dotto Madale akifafanua jambo katika Mkutano wa kuzindua Zoezi la uthamini na upimaji wa eneo la Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mkoa wa Simiyu,  uliofanyika katika Vijiji vya Igegu na Ng’arita wilayani Bariadi Septemba 14, 2018. 
Afisa Ardhi Mkuu kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Bi. Cecilia Mwing’uri akifafanua jambo katika Mkutano wa kuzindua Zoezi la uthamini na upimaji wa eneo la Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mkoa wa Simiyu, uliofanyika katika Vijiji vya Igegu na Ng’arita wilayani Bariadi Septemba 14, 2018. 
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Ng’arita katika Kata ya Sapiwi Wilaya ya Bariadi, wakinyoosha mikono yao juu kumhakikishia Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Festo Kiswaga kuonesha utayari wao wa kuachia maeneo yao kupisha Ujenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha mkoa huo, wakati wa Mkutano wa kufungua Zoezi la tathmini na upimaji wa maeneo hayo, Septemba 14, 2018. 



Hivyo makala WANANCHI WILAYANI BARIADI WARIDHIA KUACHIA MAENEO YAO KUPISHA UJENZI WA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA SIMIYU

yaani makala yote WANANCHI WILAYANI BARIADI WARIDHIA KUACHIA MAENEO YAO KUPISHA UJENZI WA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA SIMIYU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WANANCHI WILAYANI BARIADI WARIDHIA KUACHIA MAENEO YAO KUPISHA UJENZI WA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA SIMIYU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/wananchi-wilayani-bariadi-waridhia.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WANANCHI WILAYANI BARIADI WARIDHIA KUACHIA MAENEO YAO KUPISHA UJENZI WA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA SIMIYU"

Post a Comment