WAKANDARASI MIRADI YA UMEME WATAKIWA KUANZISHA YADI MAALUM

WAKANDARASI MIRADI YA UMEME WATAKIWA KUANZISHA YADI MAALUM - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAKANDARASI MIRADI YA UMEME WATAKIWA KUANZISHA YADI MAALUM, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAKANDARASI MIRADI YA UMEME WATAKIWA KUANZISHA YADI MAALUM
kiungo : WAKANDARASI MIRADI YA UMEME WATAKIWA KUANZISHA YADI MAALUM

soma pia


WAKANDARASI MIRADI YA UMEME WATAKIWA KUANZISHA YADI MAALUM


Na Veronica Simba – Chato

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewataka wakandarasi wote nchini wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini, kuwa na Yadi maalum za kuhifadhi vifaa katika maeneo wanakotekeleza miradi hiyo, ili kuondoa kisingizio cha kutowaunganishia wananchi umeme kutokana na kutokuwepo na vifaa.

Aliyasema hayo, jana Septemba 16, 2018 katika Kijiji cha Kahumo wilayani Chato, akiwa katika ziara ya kazi, ambapo pia aliwasha umeme rasmi kijijini hapo. “Kuanzia sasa nawaelekeza muwe na Yadi zenu ambapo mtahifadhi vifaa vyote vya kazi na sisi Serikali tutazikagua. Maneneja wa TANESCO kagueni Yadi hizo.”

Waziri alitaja vifaa vya kazi vinavyotakiwa kuwepo katika Yadi hizo kuwa ni pamoja na nyaya za umeme, nguzo, transfoma pamoja na mita za Luku. Aidha, akiwa katika Kijiji cha Magiri wilayani humo, ambako pia aliwasha umeme rasmi, Waziri Kalemani aliwaasa wananchi kuepukana na vishoka wakati wanapotaka kutandaziwa mfumo wa nyaya za umeme katika makazi yao.

Aliwataka wananchi kujiridhisha na uhalali wa mafundi watakaowatumia kuwatandazia mfumo wa nyaya, katika Ofisi za TANESCO zilizopo katika maeneo yao. Akifafanua, alisema majina ya mafundi wenye sifa yatatundikwa katika Ofisi hizo ili kuwarahisishia wananchi kuwatambua hivyo kuepukana na vishoka. 

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Magiri wilayani Chato, Mkoa wa Geita akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme, Septemba 16, 2018.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akiwasha umeme katika moja ya nyumba za wakazi wa Kijiji cha Kahumo wilayani Chato, Mkoa wa Geita, kuashiria kuwashwa rasmi kwa umeme kijijini humo. Tukio hilo lilifanyika Septemba 16, 2018, wakati Waziri akiwa katika ziara ya kazi.
Wananchi wa Kijiji cha Kahumo wilayani Chato, Mkoa wa Geita, wakimpokea kwa bashasha Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (mwenye shati la bluu-kulia), alipowasili kijijini hapo jana, Septemba 16, 2018, kuwasha rasmi umeme katika eneo hilo.

Waziri wa Nishati, Dkt, Medard Kalemani (kulia), akiwaonesha wananchi wa Kijiji cha Kasenga wilayani Chato, kifaa cha Umeme Tayari, kinachotumika kuunganisha umeme pasipo kutandaza mfumo wa nyaya (wiring). Waziri alikuwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme pamoja na kuzungumza na wananchi, jana Septemba 16, 2018. Pamoja naye pichani (kutoka kushoto) ni Meneja wa TANESCO Wilaya ya Chato, Nyabingiri Nyaonge na Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini katika eneo hilo, Ibrahim Saidi.



Hivyo makala WAKANDARASI MIRADI YA UMEME WATAKIWA KUANZISHA YADI MAALUM

yaani makala yote WAKANDARASI MIRADI YA UMEME WATAKIWA KUANZISHA YADI MAALUM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAKANDARASI MIRADI YA UMEME WATAKIWA KUANZISHA YADI MAALUM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/wakandarasi-miradi-ya-umeme-watakiwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAKANDARASI MIRADI YA UMEME WATAKIWA KUANZISHA YADI MAALUM"

Post a Comment