title : TUCTA yalaani taarifa ya upotoshaji ya LHRC yamtaka Mkurugenzi kufuta kauli yake.
kiungo : TUCTA yalaani taarifa ya upotoshaji ya LHRC yamtaka Mkurugenzi kufuta kauli yake.
TUCTA yalaani taarifa ya upotoshaji ya LHRC yamtaka Mkurugenzi kufuta kauli yake.
Hussein Ndubikile
Mwambawahabari
Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) limemtaka Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga kufuta kauli yake kuwa kituo hicho kimebaini vyama vya wafanyakazi havina msaada na kwamba wafanyakazi hufanya kazi kwa muda wa ziada bila malipo pamoja na kufanya bila mikataba ya ajira.
Aidha, TUCTA limesema taarifa hiyo ni upotoshaji na wanaipinga na kwamba haina chembe ya ukweli kwani inapingana na takwimu zilizopo kwenye ripoti husika.
Hatua hiyo hiyo imekuja hivi karibuni baada ya mkurugenzi huyo kusikiak akitoa kauli wakati akihojiwa na BBC News akieleza taarifa hiyo iliyoitwa ya upotoshaji.
Hayo yamesemwa leo jijini humo na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Yahaya Msigwa wakati akitoa tamko la kupinga taarifa iliyotolewa na LHRC inayoelezea utendaji kazi wa vyama hivyo nchini.
Amesema TUCTA wameisoma ripoti hiyo ya LHRC ya Muhtasari wa Haki za Binadamu na Biashara ya mwaka 2017 kwa umakini na kubaini maelezo yaliyotolewa yanapingana kabisa na ripoti ya kituo hicho.
Msigwa amebainisha kuwa vyama vya wafanyakazi vinafanya kazi kwa misingi ya sheria na kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 kama ilivyorekebishwa Ibara ya 18 na 19 wamepewa uhuru wa kutoa maoni na kujumuika kwa watu wenye masilahi yanayofanana.
Amefafanua kuwa katika ripoti ya LHRC imebainisha kuwa asilimia 74 ya wafanyakazi waliohojiwa walisema wana mikabata ya ajira, asilimia 95 ya wafanyakazi walibainisha wanafanya kazi kwa muda unaotakiwa kisheria, asilimia 73 wakibainisha mazingira ya kazi ni ya wastani, mazuri na mazuri sana.
Ripoti hiyo imebainisha kuwa asilimia 55 wamepata mafunzo ya afya na usalama kazini, asilimia 45 walikiri kuwa fidia hutolewa kwa wafanyakazi wanaoumia kazini huku asilimia 66 ya wafanyakazi walikiri kuwa na matawi ya vyma hivyo huku ripoti hiyo ikiongeza asilimia 90 waliohojiwa walisema wwanakwenda likizo kwa muda na kwamba asilimia 75 ya wafanykazi waliotembelewa walisema wana utaratibu wa ndani wa kushuhulikia matatizo yao.
Amefafanua kuwa kwenye taarifa hiyo ukurasa wa 13 kuhuusu uelewa wa sheria za kazi, haki na wajibu wa wafanyakazi LHRC walikiri wafanyakazi wana uelewa wa elimu ya juu ya umuhimu wa vyama hivyo.
Ameongeza kuwa vyama hivyo vinatimiza majukumu yake ipasavyo kwa kuwatetea wafanyakazi na kusimamia madai yao.
Kwa upande wake Mwansheria wa TUCTA, Noel Nchimbi amesema matamshi yaliyotolewa hayaendani na ukweli ulioko kwenye ripoti ya kituo hicho hivyo kinapaswa kufuta matamshi hayo.
Naye Katibu Mkuu wa Tewuta, Junus Ndalo amesisitiza kuwa kituo hicho kimepotea taarifa ya upotoshaji inavyovishushia hadhi vyama vya wafanyakazi.
Hivyo makala TUCTA yalaani taarifa ya upotoshaji ya LHRC yamtaka Mkurugenzi kufuta kauli yake.
yaani makala yote TUCTA yalaani taarifa ya upotoshaji ya LHRC yamtaka Mkurugenzi kufuta kauli yake. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TUCTA yalaani taarifa ya upotoshaji ya LHRC yamtaka Mkurugenzi kufuta kauli yake. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/tucta-yalaani-taarifa-ya-upotoshaji-ya.html
0 Response to "TUCTA yalaani taarifa ya upotoshaji ya LHRC yamtaka Mkurugenzi kufuta kauli yake."
Post a Comment