title : TMA KUCHOCHEA MATUMIZI YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KWA SEKTA MBALIMBALI ZA KIUCHUMI NA KIJAMII
kiungo : TMA KUCHOCHEA MATUMIZI YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KWA SEKTA MBALIMBALI ZA KIUCHUMI NA KIJAMII
TMA KUCHOCHEA MATUMIZI YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KWA SEKTA MBALIMBALI ZA KIUCHUMI NA KIJAMII
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeandaa mkutano wa wadau mbalimbali kwa ajili ya msimu wa mvua za Vuli (Oktoba hadi Desemba, 2018) ambao unalenga kupata maoni ya wadau jinsi utabiri wa Msimu wa Mvua za Vuli utakavyoweza kutumika katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii. Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Ushirikishwaji wa Wadau Katika Kuchochea Matumizi Ya Taarifa Za Hali Ya Hewa”.
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Dkt. Agnes Kijazi alisema kuwa lengo kubwa la mkutano huo ni kuchochea matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii hapa nchini.
‘lengo kubwa la mkutano huu kama ilivyo katika kauli mbiu ni kuchochea matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii, ambapo katika mkutano huu, mtapata fursa ya kuona utabiri wa hali ya hewa wa msimu wa Oktoba hadi Disemba, 2018 na hivyo kuwa na majadiliano yenye lengo la kuchangia juu ya athari zitakazopatikana katika sekta zenu kutokana na utabiri huo na hatimaye kuandaa mbinu na mipango ya kukabiliana na athari hizo’. Alisema Dkt.Kijazi.
Aidha aliongezea kuwa mkutano huo ni sehemu ya kubadilishana uzoefu kati ya wataalamu wa TMA, Sekta mbalimbali na Washirika wa Maendeleo hivyo basi ni sehemu muhimu ya ushirikishwaji wa wadau katika kujenga na kuimarisha utoaji na matumizi ya huduma za hali ya hewa katika jamii akisisitiza kuwa kauli mbiu imechaguliwa ili kuakisi jitihada za Mamlaka katika uandaaji na utoaji wa huduma shirikishi.
Hivyo makala TMA KUCHOCHEA MATUMIZI YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KWA SEKTA MBALIMBALI ZA KIUCHUMI NA KIJAMII
yaani makala yote TMA KUCHOCHEA MATUMIZI YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KWA SEKTA MBALIMBALI ZA KIUCHUMI NA KIJAMII Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TMA KUCHOCHEA MATUMIZI YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KWA SEKTA MBALIMBALI ZA KIUCHUMI NA KIJAMII mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/tma-kuchochea-matumizi-ya-taarifa-za.html
0 Response to "TMA KUCHOCHEA MATUMIZI YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KWA SEKTA MBALIMBALI ZA KIUCHUMI NA KIJAMII"
Post a Comment